Dec 09, 2018 02:54 UTC
  • Vibaraka wa Saudia katika mazungumzo ya Yemen washindwa kuchukua maamuzi

Afisa wa Serikali ya Uokozi wa Kitaifa Yemen katika mazungumzo ya amani ya Yemen yanaoendelea Sweden amesema kuwa, wajumbe wanaoungwa mkono na Saudia Arabia katika mazungumzo hayo hawana uwezo wa kuchukua maamuzi.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Al Masirah, Salim Al Maghlis akizungumza pembizoni mwa mazungumzo ya Wayemen-Wayemen nje kidogo ya mji mkuu wa Sweden, Stockholm, akisema  kuwa, upande wa pili katika mazungumzo hayo yaani ujumbe wa serikali iliyojiuzulu ya Abdu Rabuh Mansour Hadi, ambao ni maarufu kama  'Timu ya Riyadh' hauna uhuru wa kuchukua maamuzi. Amesema kwa kuzingatia nukta hiyo, ujumbe wa Serikali ya Uokozi wa Kitaifa, ambao ni maarufu kama "Timu ya Sanaa" utashinikiza kuwa Saudi Arabia na Imarati (UAE) zifike katika meza ya mazungumzo. Al Maghlis ameongeza kuwa, timu hiyo ya Riyadh haina uwezo wa kuchukua maamuzi kwani wanalazimika kuwafahamisha mabwana zao kwanza, yaani Saudia na Imarati kuhusu yanayojiri katika mazungumzo ili wapate maagizo kuhusu nini cha kusema.

Abdou Rabuh Mansour Hadi, rais aliyejiuzulu Yemen na ambaye ni kibaraka wa Saudia

Aidha amesema "Timu ya Sanaa" inapendekeza mapigano yote yasitishwe nchini Yemen lakini "Timu ya Riyadh" imepinga pendekezo hilo.

Al Maghlis amesema, ujumbe wa serikali iliyojiuzulu ya Abdu Rabuh Mansour Hadi ni kibaraka wa Saudi Arabia hivyo hauna uhuru wa kuamua kuhusu amani au vita.

Mazungumzo ya Wayemen-Wayemen ya kutaufata amani nchini Yemen baada ya kuanza hujuma ya Saudia Machi 2015, yalianza Ijumaa nchini Sweden kufuatia jitihada za upatanishi za Umoja wa Mataifa.

Tags