Abdul-Malik Al-Houthi: Wanaoanzisha uhusiano wa kawaida na Israel watajuta
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i83104-abdul_malik_al_houthi_wanaoanzisha_uhusiano_wa_kawaida_na_israel_watajuta
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, wanaokwenda mbio kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel watajuta kwa hatua yao hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 30, 2022 07:20 UTC
  • Abdul-Malik Al-Houthi: Wanaoanzisha uhusiano wa kawaida na Israel watajuta

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, wanaokwenda mbio kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel watajuta kwa hatua yao hiyo.

Abdul-Malik al-Houthi amesisitiza kwamba, wanaohaha huku na kule kwa ajili ya kuanzisha uhusiano na Israel ni watashindwa na mwisho wa siku watajutia hatua hiyo.

Amesema kuwa, hii leo tunashuhudia matunda mazuri ya hatua sahihi katika kukabiliana na maadui kama tunavyoshuhudia hilo huko Palestina, Lebanon na Yemen.

Kuhusiana na maadhimisho ya Quds, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah yay Yemen amesema, kuadhimishwa kwa hamasa kubwa Siku ya Kimataifa ya Quds katika ulimwengu wa Kiislamu ni jambo muhimu sana.

Maandamano ya kupinga kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel

 

Kiongozi huyo amekosoa vikali hujuma na jinai za utawala wa Kizayuuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina na kutaka kudumishwa uungaji mkono kwa wananchi hao madhulumu.

Kwa upande wake, Muhammad al-Bukhaiti, Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uachane na hatua zake za kinyama dhidi ya Baytul-Muqaddas.

Wimbi la malalamiko dhidi ya baadhi ya mataifa yaliyoanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel limekuwa likiongezeka kila siku huku mataifa hayo yakitajwa kuwa wasaliti wa kadhia ya Palestina na msikiti wa al-Aqswa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.