Ansarullah yakaribisha kuondoka Imarati huko Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i9415-ansarullah_yakaribisha_kuondoka_imarati_huko_yemen
Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amekaribisha hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ya kusimamamisha ushirikiano wake na muungano vamizi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 18, 2016 04:29 UTC
  • Ansarullah yakaribisha kuondoka Imarati huko Yemen

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amekaribisha hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ya kusimamamisha ushirikiano wake na muungano vamizi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia.

Muhammad Ali al Houthi ameunga mkono hatua ya Imarati ya kuondoa wanajeshi wake vitani huko Yemen na kuzitaka nchi nyingine wanachama wa muungano chokozi unaoongozwa na Saudia pia kuacha kuendeleza mashambulizi yao dhidi ya raia wa Yemen; mashambulizi ambayo hayana natija ghairi ya kuzidisha hasara na maafa kwa raia wa nchi hiyo.

Muhammad Ali al Houthi Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen pia ameuomba Umoja wa Mataifa kuacha kuwa mtekelezaji wa siasa za Saudi Arabia au wa nchi nyingine na badala yake kuwatetea na kuwaunga mkono wananchi madhlumu wa Yemen.

Anwar Mohammed Qarqash Waziri Mshauri wa Masuala ya Nje wa Imarati ametangaza kuwa muda wa kuhudumu vikosi vya nchi hiyo huko Yemen umemalizika.

Hii ni katika hali ambayo Saudi Arabia haijafurahishwa na hatua hiyo ya Imarati ya kuondoa wanajeshi wake huko Yemen katika kipindi hiki ambapo mazungumzo kati ya makundi ya Wayemeni bado hayajafikia natija huko Kuwait.