Dec 02, 2023 06:24 UTC
  • Kumaliza kipindi cha mfumo wa kambi moja yenye nguvu wa Marekani

Msemaji wa Kremlin amesema ulimwengu wa mfumo wa kambi moja yenye nguvu unaoongozwa na Marekani unakaribia mwisho wake.

Moja ya sababu za kumalizika udhibiti wa utawala wa Marekani duniani ni mchakato wa kutumika fedha za kitaifa katika nchi nyingi badala ya dola ya Marekani, ambao ulishika kasi baada ya kutekelezwa vikwazo dhidi ya Russia na nchi za Magharibi kwa kisingizio cha vita vya Ukraine.

Kwa mujibu wa ripoti ya Jumamosi ya Shirika la Habari la Fars, Dmitry Peskov, Msemaji wa Kremlin amesema katika mkutano na waandishi wa habari, kuwa enzi za utawala wa Marekani duniani zinakaribia mwisho wake na kuwa ulimwengu unakaribia kushuhudia mfumo tofauti wa utawala, katika nyanja za mahusiano ya kiuchumi.

Dmitry Peskov, Msemaji wa Kremlin

Peskov ameongeza kuwa: Huenda Marekani ikawa nchi iliyo na uchumi mkubwa zaidi duniani, lakini si nchi pekee yenye uchumi mkubwa ulimwenguni, na uchumi mkubwa wa dunia haudhibitiwa na Marekani pekee.

Msemaji huyo wa Kremlin amesisitiza kuwa: China ina uchumi  ambao unakaribiana na wa Marekani duniani. Uchumi unaoibuka kwingineko ambao unahitaji rasilimali za nishati unaongezeka. Dunia ina machaguo mengine tofauti mbali na Marekani.

Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, pia alisema Jumatatu iliyopita kwamba vikwazo vilivyowekewa nchi hiyo na Marekani ili kudhoofisha uchumi wake kwa hakika vimeimarisha mfumo wa pande kadhaa za nguvu katika uhusiano wa kimataifa.