Jul 14, 2024 10:09 UTC
  • Wanariadha wa Ireland waonyesha mshikamano na wananchi wa Palestina

Wanariadha wa Ireland katika mji mkuu wa nchi hiyo Dublin wameonyesha mshikamano na wananchi wa Palestina wakipinga vita na mauaji ya kimbari yanayoendelea kkufanywa na Israel Ukanda wa Gaza.

Makumi ya wanamichezo hao wa Ireland wameshiriki katika maandamano ya kuiunga mkono Palestina mbele ya jengo la Bunge la nchi hiyo. 

Eric Dovan, mwana ndondi wa zamani wa Ireland na bingwa wa zamani wa Ulaya mwenye umri wa miaka 38 amesema kuwa maandamano hayo ni muhimu sana kwa ajili ya kupaza sauti za kudai haki na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Ukanda wa Gaza. 

"Kile kinachotokea hivi sasa Ukanda wa Gaza si haki na si sawa, ni uhalifu wa kutisha na ni hatua zisizo za kibinadamu zinazotekelezwa na Israel ikisaidiwa na washirika wake huko Marekani na Ulaya," amesema Eric Dovan.

Jinai za kutisha za Israel dhidi ya watoto wasio na hatia wa Palestina 

Amesema, mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza yanapasa kusitishwa, na Palestina inapasa kuwa huru.

Katika maandamano hayo huko Dublin, kundi la waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina wakiwemo wanariadha wameonyesha kadi nyekundu wakiashiria kuwa Israel haipasi kuruhusiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya michezo. 

Tags