Sep 15, 2024 03:50 UTC
  • Medvedev: Russia ina sababu za kutumia silaha za nyuklia

Dmitry Medvedev, Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Russia, ametishia kutumia silaha zisizo za nyuklia zenye uwezo wa kuigeuza Kiev kuwa "rundo lililoyeyushwa" wakati ustahimilivu wa Moscow utakapomalizika.

Medvedev amesema kuwa nchi yake inaweza kuuangamiza kabisa mji mkuu wa Ukraine, Kiev, kwa silaha mpya zenye teknolojia ya hali ya juu katika kukabiliana na matumizi ya Ukraine ya makombora ya masafa marefu ya nchi za Magharibi.

Rais huyo wa zamani wa Russia ameeleza kuwa, nchi yake tayari ina sababu rasmi za kutumia silaha za nyuklia, lakini hadi sasa imechagua kutofanya hivyo.

Medvedev: Russia ina sababu za kutumia makombora ya nyuklia

Medvedev amekuwa akizitutumu nchi za Magharibi kuwa zinachochea vita vya nyuklia vyenye uharibifu mkubwa kwa sababu ya kuendelea kuiunga mkono kijeshi Ukraine katika vita vyake dhidi ya Russia.

Kwa upande wake balozi wa Russia mjini Washington, Anatoly Antonov, amesema kuwa Marekani haitasalimika na mzozo wowote wa nyuklia unaoweza kuzuka barani Ulaya.

Antonov ametoa wito kwa utawala wa Marekani kuacha kucheza na maneno.