Trump amteua Mrepublican mkereketwa wa Israel na adui mkubwa wa Iran kuwa balozi UN
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mbunge wa chama cha Republican Elise Stefanik, muungaji mkono mkubwa wa utawala wa Kizayuni wa Israel na mpinzani mkali wa Iran kuwa balozi ajaye katika Umoja wa Mataifa.
Mbunge huyo wa chama cha Republican amekuwa mmoja wa wakereketwa na waungaji mkono wakubwa wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakati wa vita vyake vya kinyama na mauaji ya kimbari unayoendelea kufanya dhidi ya Wapalestina wa Ghaza na dhidi ya wananchi wa Lebanon.
Stefanik aliunga mkono pia uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kulipiga marufuku Shirika la Misaada na Kazi la Umoja wa Mataifa kwa Wapalestina (UNRWA).
Mapema mwezi huu, alisikika akisema: "serikali ya Biden na Harris imetuma zaidi ya dola bilioni moja kwa ajili ya UNRWA tangu 2021, kujaza hazina ya safu hii ya kigaidi. Hili lazima likomeshwe”.../