Washiriki wa maandamano ya kuunga mkono Palestina wakamatwa Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128522-washiriki_wa_maandamano_ya_kuunga_mkono_palestina_wakamatwa_uingereza
Polisi wa Uingereza wamemkamata zaidi ya watu 50 katikati ya London wakati wa maandamano ya kupinga marufuku ya kundi la Palestine Action linalounga mkono Palestina.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jul 19, 2025 23:03 UTC
  • Washiriki wa maandamano ya kuunga mkono Palestina wakamatwa Uingereza

Polisi wa Uingereza wamemkamata zaidi ya watu 50 katikati ya London wakati wa maandamano ya kupinga marufuku ya kundi la Palestine Action linalounga mkono Palestina.

Maandamano kama hayo yalifanyika kote Uingereza, katika miji ya Manchester, Edinburgh, Bristol, na Truro siku ya Jumamosi.
Huko London, waandamanaji walikusanyika katika Uwanja wa Bunge wakibeba mabango meupe yaliyoandikwa: “Napingana na mauaji ya kimbari, naunga mkono Palestine Action.”
Polisi wa Metropolitan walisema kwenye mtandao wa X: “Watu 55 walikamatwa Uwanja wa Bunge kwa kuonesha mabango yanayounga mkono kundi la Palestine Action, ambalo limepigwa marufuku.”
Washiriki kadhaa wa maandamano hayo ya amani walikamatwa na polisi waliotumia mkono wa chuma kuwakandamiza.

Palestine Action ni kundi ambalo limekuwa likiongoza maandamano katika  viwanda vya silaha vya Uingereza ambavyo vinategeneza silaha zinazotumiwa na utawala haramu wa Israel katika vita na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.

Waandamanji wa kundi hilo wamekuwa wakimimina  rangi nyekundu nje ya viwanda hivyo vya silaha kama ishara ya namna silaha hizo zianvyotumiwa kumwaga damu ya Wapalestina wasio na hatia. Uingereza, ambayo ni muitifaki mkuu wa Israel barani Ulaya, imepitisha sheria 5 Julai kupiga marufuku kundi hilo chini ya Sheria ya Ugaidi ya mwaka 2000.
Uamuzi huo unafanya kuwa kosa la jinai kuunga mkono au kuwa mwanachama wa kundi hilo. Wanachama wa kundi hilo wanakabiliwa na adhabu ya hadi miaka 14 jela.
Shirika la Defend Our Juries, linaloratibu maandamano haya, limesema hadi sasa watu 120 wamekamatwa kote Uingereza.
Maandamano ya Jumamosi yanakuja kabla ya kesi muhimu Mahakama Kuu Jumatatu, ambapo Huda Ammori, mwanzilishi mwenza wa Palestine Action, amewasilisha kesi ya kupinga marufuku hiyo.

Uingereza ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikijinadi kuwa eti ni kitovu cha demokrasia na uhuru wa maoni sasa imegeuka kuwa utawala wa kidikteta unaokandamiza kila ambaye anashiriki katika maandamano ya amani ya kutetea Palestina na kulaani jinai za utawala dhalimu wa Israel.