Maandamano dhidi ya Trump yafanyika katika miji zaidi ya 1500 Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128524-maandamano_dhidi_ya_trump_yafanyika_katika_miji_zaidi_ya_1500_marekani
Sheria mpya ya bajeti iliyopitishwa hivi karibuni nchini marekani, inayokandamiza wananchi wa kawaida huku ikiwapa matajiri punguzo la kodi, imeongeza hasira na msongo wa kifedha, ambapo asilimia 70 ya Wamarekani wanahisi msongo mkubwa wa kifedha kuliko wakati wowote ule.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jul 19, 2025 23:04 UTC
  • Maandamano dhidi ya Trump yafanyika katika miji zaidi ya 1500 Marekani

Sheria mpya ya bajeti iliyopitishwa hivi karibuni nchini marekani, inayokandamiza wananchi wa kawaida huku ikiwapa matajiri punguzo la kodi, imeongeza hasira na msongo wa kifedha, ambapo asilimia 70 ya Wamarekani wanahisi msongo mkubwa wa kifedha kuliko wakati wowote ule.

Ili kuadhimisha miaka mitano tangu kifo mtetezi wa haki za kiraia John Lewis, maandamano yalifanyika katika miji zaidi ya 1500 kote Marekani dhidi ya sera za Rais Donald Trump na kuunga mkono urithi wa maandamano ya amani ulioangusha mfumo wa ubaguzi wa rangi Marekani miaka 60 iliyopita. Trump anashutumiwa kwa kujaribu kupunguza haki za kiraia, haki za kupiga kura, haki ya upinzani, haki za wahamiaji na mengineyo.

Mbali na kupunguzwa kwa haki hizo, kuna sheria ya bajeti iliyopitishwa hivi karibuni inayokandamiza wananchi wa kawaida ambao wanabeba mzigo wa kodi ambayo ilipaswa kulipwa na matajiri nchini humo.

Sheria hiyo inakuja wakati utafiti wa hivi karibuni ulionyesha kuwa asilimia 70 ya Wamarekani wanasema wanashughulikia msongo wa kifedha mkubwa zaidi kuliko walivyowahi kuwa.Waandamanaji wengi walikasirishwa sana na upunguzaji wa msaada wa chakula kwa maskini uliofanywa na Trump.

Asilimia ya Wamarekani wanaokumbwa na ukosefu wa chakula imefikia asilimia 16 ya nchi, idadi ambayo imeongezeka mara mbili katika miaka minne . Kwa sababu ya kampeni kali dhidi ya uhamiaji haramu na vita vilivyofeli dhidi ya Iran, kiwango cha kupingwa kwa Trump sasa kiko asilimia 55.

Uamuzi wa Trump wa kuongeza ukosefu wa usawa wa kiuchumi wakati wa hali isiyo ya kawaida ya kiuchumi unaweza kuongeza kiwango cha kupingwa kwake hata zaidi, na hivi karibuni.