Utafiti: Bei za vyakula yaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128680-utafiti_bei_za_vyakula_yaathiriwa_pakubwa_na_mabadiliko_ya_tabianchi
Imeelezwa kuwa, bei za vyakula imeathiriwa mno na mabadiliko ya tabia nchi.
(last modified 2025-07-23T23:17:07+00:00 )
Jul 23, 2025 23:17 UTC
  • Utafiti: Bei za vyakula yaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi

Imeelezwa kuwa, bei za vyakula imeathiriwa mno na mabadiliko ya tabia nchi.

Utafiti uliofanywa na mashirika mbalimbali yanayotunga sera kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, unaonesha kuwa, bei ya vyakula kama viazi, nyanya, mchele, Kabeji na vingine, imeathiriwa pakubwa kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo, katika nchi 18 kwa kipindi cha miaka miwili kati ya mwaka 2022 na 2024, ongezeko la joto na kiangazi, vimesabababisha kiwango cha mazao kushuka na hivyo bei kupanda. Kupitia ripoti iliyotolewa wakati wa kikao muhimu cha Umoja wa Mataifa, kilichofanyika nchini Ethiopia kujadili uhusiano wa kupanda kwa bei ya vyakula na mabadiliko ya tabianchi, watalaamu wameonya kuwa, mabadiliko ya tabianchi kama mafuriko ni ukame, ni kikwazo kikubwa kwa uzalishaji wa vyakula na hivyo, uhaba umesababisha bei kupanda maradufu.

Mfano nchini Ethiopia, bei ya vyakula ilipanda kwa asilimia 40, kuanzia mwaka 2022 na kuendelea hadi mwaka 2023 kwa sababu ya kiangazi kilichodumu kwa muda mrefu. Nchini Ghana na Ivory Coast, kutokana na kiangazi kilichoshuhidiwa pia kwa muda mrefu, bei ya Cocoa, ilipanda kwenye soko la imataifa kwa asilimia 280 mwezi Aprili mwaka jana (2024).