Makanisa ya Uholanzi yatangaza kuitambua Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129678-makanisa_ya_uholanzi_yatangaza_kuitambua_palestina
Makanisa 73 ya Kiprotestanti nchini Uholanzi yametoa taarifa ya kuitaka serikali ya nchi hiyo kulitambua taifa la Palestina na kuacha kupeleka shehena ya silaha kwa utawala wa kizayuni wa Israel.
(last modified 2025-08-18T07:26:49+00:00 )
Aug 18, 2025 07:26 UTC
  • Makanisa ya Uholanzi yatangaza kuitambua Palestina

Makanisa 73 ya Kiprotestanti nchini Uholanzi yametoa taarifa ya kuitaka serikali ya nchi hiyo kulitambua taifa la Palestina na kuacha kupeleka shehena ya silaha kwa utawala wa kizayuni wa Israel.

Gazeti la Uholanzi "Trav" lilichapisha taarifa na takwa lililotiwa saini na viongozi wa makanisa hayo. Katika taarifa hiyo, pamoja na kuomba kutambuliwa Palestina, serikali ya mpito ya Uholanzi imetakiwa kuchukua hatua ya kuushinikiza utawala wa kizayuni kuanzisha usitishaji vita, kuruhusu upelekaji misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, kukomesha ghasia katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kuwaachia huru mateka inaowashikilia.

Caroline Jespers, mwanzilishi wa vuguvugu hili, alisisitiza katika mahojiano na gazeti hili: "Nilikuwa na wasiwasi kuhusu hali ya Gaza kwa muda mrefu, lakini wakati ambapo Israel ilianza sera yake ya njaa ya watu wa Gaza ilikuwa ni hatua ya mabadiliko kwangu.

 Kutambuliwa kwa Palestina na Uholanzi si suala la kisiasa, bali ni hitajio la kimsingi la mwanadamu kwa taifa hili la Palestina." Mwezi Desemba mwaka jana (2024), Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio linalotaka kuwepo kwa mazungumzo ya kuaminika kwa ajili ya mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati.

Kisha uliamua kuitisha "mkutano wa ngazi ya juu wa kimataifa kwa ajili ya utekelezaji wa suluhisho la serikali mbili" huko New York mwezi Julai mwaka huu. Ufaransa na Saudi Arabia zilipewa jukumu la kuongoza mkutano huo. Hadi sasa nchi ya Palestina imetambuliwa na takriban nchi 150 duniani na kuna mataifa kadhaa ya Ulaya ikiwemo Ufaransa, Canada, Uingereza na mengineyo ambayo yamaetangaza kufanya hivyo katika mkutano mkuu ujao wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.