Israel yazuiwa kushiriki maonyesho ya biashara ya Italia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129694-israel_yazuiwa_kushiriki_maonyesho_ya_biashara_ya_italia
Utawala wa kizayuni wa Israel umepigwa marufuku kushiriki katika maonyesho ya biashaya Italia.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 18, 2025 23:36 UTC
  • Israel yazuiwa kushiriki maonyesho ya biashara ya Italia

Utawala wa kizayuni wa Israel umepigwa marufuku kushiriki katika maonyesho ya biashaya Italia.

Waandaaji wa maonyesho ya biashara ya 'Fiera del Levante' nchini Italia wameamua kutoualika utawala wa Israel kwenye maonyesho ya kila mwaka ya biashara yatakayofanyika katika mji wa Bari, Italia, mwezi Septemba ujao. Maonyesho ya kibiashara ya Fiera del Levante yamepangwa kufanyika kuanzia Septemba 13 hadi 21.

Imeelezwa kuwa uamuzi huo unatokana na Israel kuendelea kufanya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza na muendelezo wa sera yake ya kuwaua kwa njaa wakazi wa Ukanda huo kwa kuzuia kuingia misaada katika eneo hilo. Kufuatia jinai zinazofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Gaza, nchi nyingi, mashirika na shakhsia wa umma wamesisitiza kuususia utawala huo katika sekta mbalimbali.

Katika miaka ya karibuni, hasa kutokana na kushadidi mzozo wa binadamu huko Gaza, kumekuwepo wimbi kubwa la miito ya kimataifa kwa ajili ya kuigomea Israel katika michezo, jambo ambalo limeungwa mkono kikamilifu na mashirika mashuhuri ya kutetea haki za binadamu na hata baadhi ya serikali na jumuiya za kimataifa.

Mnamo Mei 2024, Shirikisho la Soka la Asia liliomba kuondolewa Israel katika Shirikisho la Soka Duniani, lakini ombi hilo bado halijapata jibu rasmi kutoka kwa FIFA. Afrika Kusini ambayo ina historia ndefu ya kupinga vitendo vya Israel na hata kuushtaki utawala wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwa kukiuka Mkataba wa Geneva wa mwaka 1948 wa Kuzuia Mauaji ya Kimbari, imetaka Israel kususiwa kimichezo.