Idadi ya Wamarekani wanaoomba hifadhi nchini Canada inaongezeka
Data za Bodi ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Canada zinaonyesha kwamba Wamarekani wengi wameomba hadhi ya ukimbizi nchini Canada katika nusu ya kwanza ya 2025 kuliko mwaka wote wa 2024, na zaidi ya mwaka wowote kamili tangu 2019.
Kwa mujibu wa data za Bodi ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Canada, watu 204 waliwasilisha maombi ya ukimbizi mwaka jana, wakitaja Marekani kama chanzo cha mateso. Maombi ya hifadhi kutoka Marekani pia yaliongezeka wakati wa utawala wa kwanza wa Rais Donald Trump.
Watafuta hifadhi kutoka nchi nyingine wanaovuka mpaka wa ardhi kutoka Marekani kwenda Canada wanarudishwa chini ya makubaliano ya nchi mbili kwa msingi kwamba lazima waombe hifadhi katika nchi ya kwanza "salama" wanayofikia.
Takwimu hizo hazitaji sababu ya maombi hayo, lakini Reuters ilinukuu mawakili wanane wakisema kuwa Wamarekani waliobadili jinsia wanataka kuondoka nchini mwao.
Ili kupewa hifadhi ya ukimbizi, waombaji lazima waishawishi Bodi ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Canada kwamba Marekani si salama kwao.