Mogherini: Ujenzi wa vitongoji vya Israel ni kinyume cha sheria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i24799-mogherini_ujenzi_wa_vitongoji_vya_israel_ni_kinyume_cha_sheria
Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya alisisitiza jana huko Brussels kuwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi unaofanywa na utawala wa Kizayuni ni kinyume cha sheria na kwamba Umoja wa Ulaya hauafiki ujenzi huo wa vitongoji.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 07, 2017 03:35 UTC
  • Mogherini: Ujenzi wa vitongoji vya Israel ni kinyume cha sheria

Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya alisisitiza jana huko Brussels kuwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi unaofanywa na utawala wa Kizayuni ni kinyume cha sheria na kwamba Umoja wa Ulaya hauafiki ujenzi huo wa vitongoji.

Nikolay Mladenov Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Mashariki ya Kati alisema jana kuwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unakiuka sheria za kimataifa.

Nikolay Mladenov, Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa UN katika Mashariki ya Kati 

 Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa umebainisha wasiwasi wao kufuatia kuendelea ujenzi wa vitongoji wa Israel ambao ni kinyume cha sheria katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu katika hali ambayo bunge la utawala wa Kizayuni (Knesset) jana lilipasisha mswada uliozusha makelele wa kuufanya halali ujenzi wa vitongoji vya walowezi huko katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Mswada huo unaandaa uwanja wa kuendelezwa ujenzi huo wa vitongoji kinyume cha sheria katika eneo hilo.

Kiburi cha viongozi wa utawala ghasibu wa Kizayuni hivi sasa kimeongezeka zaidi baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump wa Marekani; huku utawala huo kila siku ukiidhinisha miradi mipya ya kujenga vitongoji katika ardhi za Wapalestina licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwasilisha azimio hivi karibuni linaloitaka Israel isimamishe ujenzi huo wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi.