Mar 19, 2016 02:56 UTC
  • Wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la ubaguzi duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amebainisha wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la ubaguzi na ghasia inayohusiana na chuki za kibaguzi duniani kote.

Maoni hayo ameyatoa akihutubia kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Ijumaa kwa ajili ya siku ya kutokomeza ubaguzi wa rangi, ambayo itaadhimishwa tarehe 21 Machi.

Ban ameaanza kwa kupongeza hatua zilizofikiwa katika kuhakikisha usawa wa haki na kutokomeza ubaguzi, tangu mauaji ya waandamanaji dhidi ya ubaguzi wa rangi, mjini Sharpeville, Afrika Kusini, tarehe 21, Machi, mwaka 1960.

Hata hivyo amesema mzozo na mivutano dhidi ya vikundi vya watu walio wachache imeongezeka, akimulika hasa ghasia, chuki na mashambulizi dhidi ya wahamiaji, wakimbizi na Waislamu.

"Vyama vya kisiasa venye itikadi kali vinachochea mgawanyiko wa jamii na kuongeza hatari, na sauti zilizokuwa na busara zamani sasa zinachochea hofu, ikikumbusha nyakati mbaya za historia ya karne iliyopita. Hayo yote yanaongeza hatari ya kuvunjwa kwa mshikamano wa jamii, ukosefu wa utulivu na mizozo."

Katibu Mkuu amesisitiza kwamba mashambulizi dhidi ya kundi moja ni sawa na mashambulizi dhidi ya wote, akisema ni lazima kudumisha haki na utu kwa wote.

Hayo yanajiri wakati ambao hivi karibuni Waislamu nchini Marekani, walisema kuwa maneno ya chuki dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu yanayotolewa na viongozi wa chama cha Republican, ndiyo sababu ya kuongezeka hujuma na mashambulizi dhidi ya Waislamu nchini humo. imemtaka Donald Trump, anayewania kuteuliwa na chama cha Republican kugombea urais nchini Marekani, amekuwa akitoa matamshi makali dhidi ya Waislamu. Kwa ujumla kumeshuhudiw akuongezeka chuki dhidi ya Waislamu kote duniani kutokana na sera za nchi za Magharibi za kuuchafulia jina Uislamu na Waislamu.

Tags