Philip Roth: Rais Trump ni mtu mwongo na mpumbavu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i34487-philip_roth_rais_trump_ni_mtu_mwongo_na_mpumbavu
Mwandishi mmoja wa Kimarekani amemshambulia kwa maneno makali Rais Donald wa Marekani na kumuita kuwa ni mtu mwongo na mpumbavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 17, 2017 09:36 UTC
  • Philip Roth: Rais Trump ni mtu mwongo na mpumbavu

Mwandishi mmoja wa Kimarekani amemshambulia kwa maneno makali Rais Donald wa Marekani na kumuita kuwa ni mtu mwongo na mpumbavu.

Philip Roth ambaye ni mwandishi wa riwaya na simulizi amesema kuwa, Trump ni mtu mwongo, mpumbavu na asiyejua kitu. Akizungumza katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeli la Kifaransa la Liberacion, Philip Roth amesema kuwa, Donald Trump anasumbuliwa na maradhi ya kujiona kupita kiasi, na ni mtu muongo kwa maana halisi ya neno na ni mjinga asiyejua kitu. 

Aidha mwandishi huyo wa simulizi wa Kimarekani amesema kuwa, Trump ana moyo wa chuki na sifa ya ulipizaji kisasi.

Philip Roth amesema kuwa, vitendo vya ajabu ajabu vya Rais Trump, kutokuwa kwake na uzoefu na kutoa matamshi yasiyostahiki ni mambo ambayo yamewaudhi na kuwakera mno Wamarekani.

Amesema kuwa, yumkini Marekani na ulimwengu ukakumbwa na hasara kubwa kutokana na ukosefu wa busara wa rais huyo wa sasa wa Marekani.

Philip Roth, mwandishi wa riwaya wa Marekani

Itakumbwa kuwa, huyu si mtu wa kwanza nchini Marekani kumtuhumu hadharani Rais wa Marekani kwamba, ni muongo na mtu mjinga.

Mwezi Juni mwaka huu, James Comey Mkuu wa zamani wa Polisi ya Federali ya Marekani (FBI) alinukuliwa akisema kuwa Rais Donald Trump wa nchi hiyo ni mrongo na kidhabi.

Shakhsia mbalimbali wa kisiasa wamekuwa wakimkosoa Rais wa sasa wa Marekani kutokana na kutoa matamshi ya ajabu ajabu na hata wengine kufikia kutilia shaka uwezo wake wa akili.