Rais wa Marekani awasili Cuba katika safari ya kihistoria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i3472-rais_wa_marekani_awasili_cuba_katika_safari_ya_kihistoria
Rais Barack Obama wa Marekani amewasili katika mji mkuu wa Cuba, Havana katika safari inayotajwa kuwa ya kihistoria.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 21, 2016 02:23 UTC
  • Rais wa Marekani awasili Cuba katika safari ya kihistoria

Rais Barack Obama wa Marekani amewasili katika mji mkuu wa Cuba, Havana katika safari inayotajwa kuwa ya kihistoria.

Katika safari hiyo Obama alitazamiwa kukutana na mwenyeji wake wa Cuba, Raul Castro na wawakilishi wa sekta binafsi. Vilevile atahutubia Wacuba katika jutihada za kuimarisha uhusiano wa kawaida kati ya maadui hao wawili wakubwa wa kipindi cha Vita Baridi.

Uhusiano wa Marekani na Cuba ulikatwa zaidi ya nusu karne iliyopita.

Obama anakuwa rais wa kwanza aliyeko madarakani wa Marekani kutembelea Cuba baada ya kipindi cha miaka 90.

Rais Raul Castro wa Cuba na Barack Obama walikutana kwa mara ya kwanza katika mazishi ya shujaa wa uhuru wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela na tangu wakati huo bendera ya Cuba ilipeperushwa tena katika ubalozi wa nchi hiyo mjini Wqshington baada ya kipindi cha miaka cha miaka 54.