Wanamichezo wa Marekani wapinga matamshi ya Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i34827-wanamichezo_wa_marekani_wapinga_matamshi_ya_trump
Wachezaji wa Ligi ya mchezo wa Ragbi, soka (NFL) na mpira wa kikapu (NBA) wa Marekani wameingia ulingoni kupinga matamshi ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo.
(last modified 2026-04-26T10:08:53+00:00 )
Sep 25, 2017 04:43 UTC
  • Wanamichezo wa Marekani wapinga matamshi ya Trump

Wachezaji wa Ligi ya mchezo wa Ragbi, soka (NFL) na mpira wa kikapu (NBA) wa Marekani wameingia ulingoni kupinga matamshi ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo.

Wamarekani weusi wa mchezo wa ragbi walionesha upinzani wao jana katika uwanja wa Wembley mjini London kwa kupiga magoti wakati ulipopigwa wimbo wa taifa wa Marekani. 

Upinzani wa sasa wa wanamichezo wa Marekani umeshika kasi baada ya hotuba ya juzi Ijumaa ya Donald Trump huko Huntsville katika jimbo la Alabama alipowatusi kwa maneno machafu wachezaji wanaolalamika kupinga ubaguzi wa rangi na kuwataka wamiliki wa vilabu vinavyocheza katika ligi ya NFL kuwafukuza wachezaji weusi wa nchi hiyo wanaopinga ubaguzi wa rangi kwa kupiga magoti wakati wimbo wa taifa unapopigwa. 

Ntota wa mpira wa kikapu Marekani, Stephen Curry amekataa mwaliko wa Trump

Matamshi hayo ya kijuba ya Rais wa Marekani yamepingwa na kushambuliwa vikali ya wachezaji mashuhuri wa soka na mpira wa kikapu wa Marekanin kama LeBron James na Bruce Maxville.

Vilevile nyota wa timu ya Golden State Warriors katika ligi ya mpira wa kikapu ya NBA, Stephen Curry amekataa mwaliko wa Rais Donald Trump huko White House kupinga sera za kibaguzi za kiongozi huyo.

Wachezaji wa ligi ya FNL wakipinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani

Harakati hiyo ya kupinga ubaguzi dhidi ya Wamarekani weusi kwa kipiga magoti wakati wimbo wa taifa wa nchi hiyo unapopigwa ilianzishwa na mchezaji wa soka la Marekani, Colin Kaepernick mwezi Agosti mwaka 2015.