Nov 30, 2022 03:07 UTC
  • Nchi za Ulaya za Mediterenia zimeshindwa kuzuia kutokea majanga ya baharini

Mkuu wa ofisi ya Masuala ya Bahari katika shirika la World Nature Foundation amesema kuwa nchi za Ulaya za Mediterenia zimeshindwa kuzuia kutokea majanga ya baharini.

Antonia Leroy Mkuu wa ofisi ya Masuala ya Bahari katika shirika la World Nature Foundation amesema kuwa: nchi tano kati ya nane za Ulaya za Mediterenia zimeshindwa kuwasilisha mipango yao kwa Kamisheni ya Ulaya kwa ajili ya shughuli endelevu katika bahari ya Mediterenia; suala ambalo linaweza kusababisha maafa ya baharini katika bahari hiyo.  

Taka za baharini 

Bahari ya Mediterenia pamoja na kuwa inawakilisha chini ya asilimia moja ya bahari duniani lakini inahesabiwa kuwa makazi ya kiumbe kimoja cha kati ya kumi vya baharini vinavyojulikana. 

Ajali za kugongana meli, taka za baharini, upotevu wa makazi, miradi ya maendeleo, shughuli za uvuvi wa kupita kiasi ni baadhi tu ya mambo ambayo yameathiri na kuharibu pakubwa mazingira ya bahari ya Mediterenia. 

Tags