Argentina bingwa wa soka Kombe la Dunia 2022
Timu ya taifa ya soka ya Argentina imetwaa Kombe la Dunia 2022 baada ya kuwasinda mabingwa watetezi Ufaransa kwa mikwaju ya penalti.
Argentina ikiongozwa na nahodha wake machachari Lionel Messi waliuanza mchezo wakiwa na usongo na kutawala dakika za awali za mchezo huo. Mabingwa hawa wapya wa soka wa Kombe la Dunia mwaka huu 2022 Qatar iliwachukua dakika 23 tu kupachika bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti kupitia nahodha wake Lionel Messi. Dakika ya 36 Angel Di Maria alipachika bao la pili na kuhuisha matumaini ya nchi yake kutwaa Kombe la Dunia. Timu mbili zilienda mapumziko huku Agrentina ikiongoza kwa mabao hayyo mawili.
Kipindi cha pili wakati zikiwa zimebakia dakika 10 kabla ya muda wa kawaida kumaliza mambo yaligeuka ghafla baada ya kinda Kylian Mbappe kupachika mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za 80 na 81. Mpambano huo ulilazimika kuendelea hadi dakika za nyongeza baada ya kutopatikana mshindi.
Kama vile ushindani ulikuwa baina ya Messi na Mbappe kwani dakika ya 108 alikuwa Messi tena aliyetikisha nyavu za Ufaransa na kuandika bao la tatu. Hata hivyo mshambuliaji hatari wa Ufaransa Kyylian Mbappe alifuta tena matumaini ya Argentina ya kutwaa kombe hilo baada ya kusawazisha kwa njia ya tuta. Hadi dakika 120 zinamalizika matokeo yalikuuwa 3-3. Ni katika upigaji penalti ndipo Argentina walipeleka habari ya msiba huko Ufaransa na kumuacha hoi Rais Emmanuel Macron wan chi hiyo aliyekuwa uwanjani akiwashuhudia vijana wake.
Mbappe amekuwa mfungaj bora wa mashindano hayo baada ya kupachika wavuni mabao 8 akiafuatiwa na Messi aliyetikisha nyavu mara saba.