Onyo kuhusu ongezeko la vijasumu sugu (superbacteria)
https://parstoday.ir/sw/news/world-i93916-onyo_kuhusu_ongezeko_la_vijasumu_sugu_(superbacteria)
Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu ongezeko la bakteria sugu (superbacteria) duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 11, 2023 03:54 UTC
  • Onyo kuhusu ongezeko la vijasumu sugu (superbacteria)

Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu ongezeko la bakteria sugu (superbacteria) duniani.

Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti yake kwamba kuna ushahidi kwamba mazingira yana jukumu muhimu katika kustawi, maambukizi na kuenea kwa bakteria sugu kwa dawa (AMR).

Umoja wa Mataifa unahusisha takriban vifo milioni moja laki mbili na sabini elfu mwaka 2019 na magonjwa sugu yasiyokubali dawa.

Shirika hilo la kimataifa limeonya kwamba vijidudu maradhi hao sugu wanaweza kuua watu milioni 10 kufikia 2050.

Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba ni muhimu kupunguza uchafuzi katika uzalishaji wa dawa na bidhaa za kilimo ili kupambana na kuenea kwa superbacteria zinazokinzana na dawa.

Ingawa matumizi ya kupita kiasi ya viuavijasumu ni sababu muhimu katika usugu wa vijasumu, Umoja wa Mataifa unasema kuwa mambo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, kutoweka kwa viumbe hai na maliasili, pamoja na uchafuzi wa mazingira na uzalishaji taka una athari za moja kwa moja katika kuzalisha vijasumu sugu (superbacteria).