Lavrov: Nchi za Magharibi zinataka makabiliano na Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i95870
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa uhusiano wa Umoja wa Ulaya mkabala wa Russia si wa kirafiki.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 04, 2023 07:03 UTC
  • Lavrov: Nchi za Magharibi zinataka makabiliano na Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa uhusiano wa Umoja wa Ulaya mkabala wa Russia si wa kirafiki.

Sergei Lavrov amesema kuhusu uhusiano wa Russia na Umoja wa Ulaya kuwa, Russia inautambua Umoja wa Ulaya kama muungano usio rafiki. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia aidha amesisitiza kuwa uhusiano dhaifu wa Umoja wa Ulaya na Moscow ni suala ambalo limesababishwa na nchi wanachama wa umoja huo kupitia uungaji mkono wao wa silaha na kuipatia washauri serikali mtenda jinai huko Kiev.  

Lavrov ameongeza kusema kuwa, iwapo italazimika Moscow itachukua hatua kujibu hatua za uhasama kwa mujibu wa maslahi ya taifa ya Russia na kulingana na kanuni zinazochukuliwa katika uga wa kidiplomasia. 

Amesema nchi za Magharibi haziko tayari kufanya mazungumzo na Moscow bali zinatafuta njia mpya za kuiwekea vizingiti Moscow. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa Marekani ni chanzo kikuu cha kutekelezwa sera dhidi ya Russia.  

Josep Borell Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya aliwahi kudai kuwa Russia inakiuka mara kwa mara fremu ya sheria za Umoja wa Mataifa licha ya kuwa mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN na kwamba Umoja wa Ulaya utasimama imara mkabala wa hatua yoyote ya kutumia vibaya nafasi ya uwenyekiti ya Russia. 

Josep Borell, Mkuu wa Sera za Nje wa EU 

Rais wa  Vladimir Putin wa Russia alianzisha operesheni ya kijeshi dhidi ya Ukraine mnamo Februari 24 mwaka 2022, akizikosoa nchi za Magharibi kwa kupuuza wasiwasi wa Moscow kuhusu usalama wa ardhi ya Russia.