Kukosoa China vigezo vya kindumakuwili katika kukabiliana na ugaidi
Zhang Jun, balozi na mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amekosoa vikali vigezo vya kindumakuwili vya Marekani kuhusiana na suala la kukabiliana na ugaidi na kueleza kwamba, ugaidi bado ni changamoto muhimu ambayo inatishia amani na usalama wa kimataifa.
Akihutubia katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, balozi Zhang Jun amesema, kuna haja ya kuweko ushirikiano wa kimataifa katika uga wa kukabiliana na hali tete ya kupambana na ugaidi na kwamba, China inaunga mkono nafasi muhimu na nyeti ya Umoja wa Mataifa katika kuratibu juhudi za mataifa ya dunia kwa ajili ya kupambana na ugaidi, kwani inaamini kuwa, hakuna ugaidi mbaya na mzuri.
Suala ala ugaidi mbaya na mzuri lilianza kuzungumziwa baada ya shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001 nchini Marekani ambapo waliowegi wanaamini kwamba, Marekani inatumia hila na mbinu hii ya kuugawa ugaidi katika makundi mawili ya ugaidi mbaya na mzuri ili kuendeleza undumakuwili wake katika suala zima la ugaidi.
Kwa kuzingatia kwamba, hakuna fasili na maana moja ya kimataifa iliyotolewa kuhusiana na ugaidi, duru za Kimagharibi hususan Marekani kila mara inapoona harakati fulani ya utumiaji mabavu ambayo ni kwa maslahi yake, huwa haitambui harakati na kitendo hicho kwamba, ni ugaidi. Lakini kinyume, pale kunapofanyika harakati za ukombozi ambazo zinatishia uhai na uwepo wa utawala ghasibu wa Israel, hulitambulisha hilo kuwa ni ugaidi.
Lee Van Ti, mweledi wa masuala ya kimataifa anasema kuhusiana na hili kwamba: Marekani ina unafiki na undumakuwili katikka masuala yote ya kimataifa likiwemo suala la nyuklia na ugaidi. Kwa maneno bora na ya wazi zaidi ni kwamba, Marekani hutoa maana ya kitu fulani kama ugaidi katika fremu ya manufaa na maslahi yake na kadiri jambo hilo linavyotishia maslahi ya Marekani basi hufanya hima na idili kwa mbinu mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana nalo, na hii leo kadhia ya ugaidi ni mfano na kielelezo cha wazi cha kadhia hii.
Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa akasisitiza pia kwamba, kujikita Marekani katika kupambana na makundi ya kigaidi ambayo ni tishio kwa Washington na kufumbia jicho makundi mengine ya kigaidi ambayo yanatoa pigo kwa mataifa mengine, ni mfano na kielelezo cha wazi cha unafiki na undumakuwili wa madola ya Magharibi hususan Marekani katika suala zima la kupambana na ugadi.
Katika miaka ya hivi karibuni hususan baada ya mwaka 2001 na kuendelea, ugaidi umekuwa ukitumiwa kama wenzo wa Marekani ambapo ikitumia kisingizio cha kupambana na ugaidi imekuwa ikiingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine. Kwa muktadha huo na kwa mtazamo wa China, kutumia suala la ugaidi kwa ajili ya kuingilia masuala ya ndani ya mataifa mengine, ni mfano na kielelezo kingine cha wazi cha undumakuwili wa Marekani ambapo tunaweza kuashiria hatua ya Washington ya kuishambulia kijeshi Afghanistan mwaka 2001.
Kwa msingi huo, Umoja wa Mataifa ukiwa taasisi kubwa zaidi ya kimataifa ili kusaidia juhudi za kuhakikisha amani na utulivu vinapatikana duniani ambapo hilo ni moja ya malengo yake makuu ya kuasisiwa kwake, inapaswa kutoa fasili na maana moja ya ugaidi ambayo itakuwa imeafikiwa na walimwengu wote.
Kuhusiana na mkakati wa kimataifa wa kupambabna na ugaidi, mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, majibu dhidi ya vitisho vya ugaidi hayapaswi kuwa ya kidhahir na kijujuuu bali yanapaswa kujikita katka kung'oa mizizi ambayo inalea na kukuza ugaidi.
Kwa msingi huo vyanzo vya kupambana na ugaidi katika Umoja wa Mataifa vinapaswa kuelekea upande wa mataifa ambayo yapo mstari wa mbele katika kupambana na ugaidi. Marekani ikitumia madai ya kupambana na ugaidi imefanya mauaji ya kutisha na umwagaji damu mkubwa katika mataifa ya Afghanista, Iraq, Syria na Yemen ikishirikiana na washirika wake na kufanya uharibfu mkubwa katika nchi hizo kama ambavyo wananchi wa mataifa hayo wangali ni wahanga wa ugaidi unaoungwa mkono na Washington. Hii ni katika hali ambayo, asasi zinazojulikana kama eti za kutetea haki za binadamu zimenyamazia kimya jinai zilizofanywa na zinazofanywa na Marekani katika maeneo mbalimbali ya dunia.