Algeria: Umoja wa Mataifa hauna uwezo wa kuwatetea wanaokandamizwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i99584-algeria_umoja_wa_mataifa_hauna_uwezo_wa_kuwatetea_wanaokandamizwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amesema, Umoja wa Mataifa hauwezi tena kuwasaidia watu wanaodhulumiwa duniani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 06, 2023 07:29 UTC
  • Algeria: Umoja wa Mataifa hauna uwezo wa kuwatetea wanaokandamizwa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amesema, Umoja wa Mataifa hauwezi tena kuwasaidia watu wanaodhulumiwa duniani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ahmed Attaf alisema jana Jumatano katika kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Uupande Wowote (NAM) kwamba Umoja wa Mataifa hauwezi tena kudhamini msaada kwa wanyonge wanaodhulumiwa duniani na kuwa kimbilio lao. Amesema Harakati ya Nchi Zisizofungana na Siasa za Upande Wowote ina majukumu ya kihistoria na lazima itimize majukumu yake ya kisiasa.

Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote ulianza jana, Jumatano, huko Baku, mji mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan, na unaendelea kwa siku 2.

Akifungua mkkutano huo, Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan amesema Ufaransa ni moja ya nchi ambazo zinaendelea kung'angania na kutekeleza sera ya ukoloni mamboleo.

Askari wa Ufaransa wakiwakandamiza waandamanaji mjini Paris

Rais wa Azerbaijan amesema amesisitiza kuwa, Rais Emmanuel Macron anapaswa kuziomba radhi nchi ambazo ziliathiriwa na ukoloni wa Ufaransa.

Amemhutubu Rais wa Ufaransa kwa kusema, "Waombe radhi mamilioni ya watu ambao watangulizi wako waliwakoloni, kuwafanya watumwa, kuwaua, kuwatesa na kuwadhalilisha."