Oct 29, 2023 22:57 UTC
  • Jumatatu, Oktoba 30, 2023

Leo ni Jumatatu tarehe 14 Rabiuthani 1445 Hijria inayosadifiana na tarehe 30 Oktoba 2023.

Siku kama ya leo miaka 1379 iliyopita Mukhtar bin Abi Ubaida al-Thaqafi alianza mapambano ya kulipiza kisasi cha damu ya Imam Hussein bin Ali (a.s), mjukuu wa Mtume Muhammad SAW.

Mwaka 61 Hijria Imam Hussein (as) akiwa pamoja na wafuasi na watu wa familia yake, aliuawa shahidi na jeshi la Yazid akiwa katika harakati za kuilinda dini tukufu ya Uislamu. Mukhtar alianzisha harakati zake za mapambano katika mji wa Kufa.

Kabla yake, kulijitokeza kundi la 'Tawwabiin' ambalo lilipigana na utawala wa Bani Umayyah, kwa lengo la kulipiza kisasi cha damu ya Imam Hussein AS. Mukhtar Thaqafi alitawala Kufa kwa kipindi cha karibu mwaka mmoja na mwishowe alishindwa na jeshi la Mus'ab bin Zubair na kuuawa shahidi.

Kaburi la Mukhtar al Thaqafi

Miaka 113 iliyopita katika siku kkama ya leo ya tarehe 30 Oktoba 1910 alifariki dunia Henry Dunant, mwasisi wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu.

Dunant alizaliwa Geneva, Uswisi na mwaka 1828, aliamua kuanzisha Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu kwa shabaha ya kuokoa maisha ya majeruhi wa vita.

Kutokana na hatua yake hiyo ya kibinadamu, Henri Dunant alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1901, na alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

هانری دونان

Katika siku kama ya leo miaka 43 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 8 Aban 1359 Hijria Shamsia, aliuawa shahidi Muhammad Hussein Fahmideh, kijana shujaa wa Kiirani kwenye vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na Iraq dhidi ya Iran.

Shahidi Fahmideh alielekea kwenye medani ya vita akiwa na umri wa miaka 13 tu, ikiwa imepita miezi michache tu baada ya kuanza kwa vita hivyo. Shahidi Fahmideh alijitolea mhanga kwa kujifunga kiunoni maguruneti na kujilaza mahala kilipokuwa kikipita kifaru cha adui na kuwatia kiwewe na hatimaye kuwalazimisha wavamizi kukimbia.

Hatua hiyo ilipongezwa na Imam Khomeini ambaye alimtaja kijana huyo kuwa ni kiongozi na kigezo cha kuigwa.

Muhammad Hussein Fahmideh