Nov 03, 2023 23:03 UTC
  • Jumamosi, 04 Novemba, 2023

Leo ni Jumamosi 19 Mfunguo Saba Rabiu Thani 1445 Hijria mwafaka na tarehe 4 Novemba 2023 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 59 iliyopita, askari vibaraka wa utawala wa Shah uliokuwa ukitawala Iran waliivamia nyumba ya kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Ruhullah Khomeini mjini Qum na kumtia mbaroni. Baada ya kumhamishia mjini Tehran, utawala wa Shah ulimbaidishia Imam Khomeini nchini Uturuki. Utawala wa Shah uliamua kufanya hivyo kutokana na uungaji mkono wa Imam Khomeini kwa harakati za mapambano za wananchi Waislamu wa Iran za kutaka kujitawala, uhuru na kutetea thamani za Kidini. Lengo la kumpeleka uhamishoni Imam Khomeini lilikuwa kusimamisha mapambano yake na wananchi Waislamu wa Iran dhidi ya utawala huo kwani utawala wa Shah ulitambua kwamba kuwepo Imam nchini kunawaamsha wananchi dhidi ya utawala huo wa kidikteta. ***

Kubaidishwa Imamu Khomeini (MA)

 

Miaka 45 iliyopita na katika siku kama ya leo yaani tarehe 13 Aban mwaka 1357 Hijria Shamsia, kulifanyika maandamano makubwa ya wanafunzi na wanachuo mjini Tehran. Maandamano hayo ya yalikandamizwa vibaya na askari wa utawala wa Shah na kusababisha umwagaji damu mkubwa. Katika siku kama hii ambayo ilisadifiana na kumbukumbu ya kubaidishwa Imam Khomeini huko Uturuki, kundi kubwa la wanafunzi na wanachuo, wakiwa na lengo la kulaani kitendo hicho cha mfalme Shah walikusanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran. Askari wa utawala wa Shah walishambulia kundi hilo la wanachuo na wanafunzi na kuwauwa shahidi wanafunzi na wanachuo wengi. Tarehe 13 Aban ina umuhimu mkubwa katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu, na ndio maana imepewa jina la "Siku ya Mwanafunzi." ***

Siku ya Mwanafunzi

 

Siku kama ya leo 44 iliyopita, wanafunzi na wanachuo wa Tehran walifanya maandamano makubwa katika mji huo kwa mnasaba wa kukumbuka tukio la kupelekwa uhamishoni nchini Uturuki Imam Khomeini MA na kwa mnasaba wa kutimia mwaka mmoja tangu kuuawa wanafunzi na wanachuo wa Iran. Mauaji hayo yalifanywa na vikosi vya usalama vya utawala wa Shah. Wanafunzi na wanachuo kadhaa wa Kiislamu walioshiriki kwenye maandamano hayo ambao walikuwa wakijulikana kama Wafuasi wa Sera za Imam, waliuvamia ubalozi wa Marekani mjini Tehran, ambao ulikuwa pango la ujasusi dhidi ya wananchi wa Iran. ***

Kutekwa pango la ujasusi la Marekanii

 

Miaka 28 iliyopita katika siku kama hii ya leo Yitzhak Rabin, Waziri Mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel aliuawa na Mzayuni mwenye misimamo ya kufurutu ada. Rabin alikuwa Waziri Mkuu wa Israel kuanzia mwaka 1974 hadi 1977 kwa tiketi ya Chama cha Leba. Hata hivyo aliuzuliwa wadhifa huo kwa tuhuma za ubadhirifu. Ni muhimu kukumbusha kuwa, Yitzhak Rabin alikuwa miongoni mwa makamanda wa makundi ya kigaidi ya Kizayuni. **

Yitzhak Rabin, Waziri Mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel