Nov 25, 2023 22:50 UTC
  • Jumapili, 26 Novemba, 2023

Leo ni Jumapili 12 Mfunguo Nane Jamadul-Awwal 1445 Hijria mwafaka na tarehe 26 Novemba 2023 Miladia.

Katika siku kama ya leo miaka 492 iliyopita alifariki dunia msomi mkubwa wa Kiislamu Ibn Tulun Dimashqi, aliyekuwa faqihi, mwanafasihi na mwanahistoria huko mjini Damascus, Syria. Ibn Tulun alizaliwa mwaka 880 Hijiria mjini Damascus na katika umri wake wote alifanya jitihada kubwa za utafiti, kufundisha na kuandika vitabu vya taaluma mbalimbali. Ibn Tulun Dimashqi ameandika vitabu vingi vya thamani kuhusiana na historia ya Kiislamu na pia katika uwanja wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu, hadithi, lugha, tiba na irfani. Aidha kitabu cha 'as-Safiinatu al-Tuluuniyyah' ni miongoni mwa athari za mwanazuoni huyo. ***

Ibn Tulun Dimashqi,

 

Katika siku kama ya leo miaka miaka 168 iliyopita, Adam Bernard Mickiewicz mshairi na mwandishi mkubwa wa Kipoland aliaga dunia huko Istanbul uliokuwa mji mkuu wa utawala wa Othmania. Alizaliwa mwaka 1798. Kama alivyokuwa baba yake, Mickiewicz naye alikuwa mtu aliyekuwa akipigania uhuru. Aliishi katika zama ambazo nchi yake ya Poland ilikuwa imegawanywa na madola ya Prussia, Russia na Austria na alikuwa akifanya jitihada ili nchi yake iungane tena na kuwa kitu kimoja. Ni kutokana na sababu hiyo ndiyo maana mwaka 1823 alibaidishiwa nchini Russia. Baada ya miaka 6, Adam Mickiewicz alikimbilia nchini Ufaransa na kuanza kufundisha fasihi ya lugha. ***

Adam Bernard Mickiewicz

 

Siku kama ya leo miaka 45 iliyopita, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 Ayatullah Muhammad Gharawi Kashani, msomi mkubwa wa sheria za Kiislamu (fiqhi) na mwanamapambano mkubwa wa wa ulimwengu wa Kiislamu nchini Iran. Alizaliwa mjini Kashan, moja ya mikoa ya katikati mwa Iran katika familia ya elimu na watu wa fadhila. Baada ya kuhitimu masomo yake ya msingi msomi huyo mkubwa alianza kusoma elimu ya dini mjini Kashan na Isfahan ambapo baada ya hapo alielekea mjini Najaf, Iraq kwa ajili ya kuendelea zaidi na masomo. Akiwa mjini Najaf, Ayatullah Muhammad Gharawi Kashani alipata kusoma kwa maulama wakubwa wa mji huo. Aidha alimu huyo hakutenganisha katu kati ya elimu na dini na daima aliamini kuwa ni mambo yasiyokubali kutengana. Mbali na kuwalea wanafunzi, pia alikuwa akipambana vikali na utawala wa kidikteta wa Shah. ***

Ayatullah Muhammad Gharawi Kashani,

 

Siku kama ya leo miaka 44 iliyopita, jeshi la kujitolea la wananchi (Basiji Mustadhaafina) liliundwa kutokana na amri ya Imam Khomeini mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuundwa jeshi la watu milioni 20 nchini Iran. Taasisi hiyo ya wananchi kutoka matabaka mbalimbali ya kijamii, kwa kuwa na wapiganaji wenye imani, moyo wa kujitolea na ari ya kuchapakazi imekuwa na nafasi muhimu katika matukio mbalimbali ya Mapinduzi ya Kiislamu hasa kipindi chote cha vita vya kujihami kutakatifu vya taifa la Iran dhidi ya uvamizi wa Iraq. Jeshi la Basiji bado linashiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiutamaduni na kijeshi hapa nchini Iran. ***

jeshi la kujitolea la wananchi (Basiji Mustadhaafina)

 

Katika siku kama ya leo miaka 33 iliyopita, Ustadh  Sayyid Hassan Mirkhani, mmoja wa waalimu hodari wa Sanaa ya hati na maandishi ya kuvutia wa Iran aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 80. Baada ya kuhitimu masomo yake ya awali alijifunza Sanaa ya hati kwa walimu mahiri wa Iran katika fani hiyo. Kwa muda mfupi Mirkhani aliweza kufikia daraja ya ualimu katika Sanaa hiyo na kisha akaanza kufundisha. Ustadh Mirkhani alikuwa na kipaji maalumu katikak Sanaa ya hati huku akiwa stadi pia katika utunzi wa mashairi. ***

Ustadh Sayyid Hassan Mirkhani