Jumatano, 12 Juni 2024
Leo ni Jumatano tarehe 5 Mfunguo Tatu Dhul-Hija 1445 Hijria ambayo inasadifiana na tarehe 12 Juni 2024 Miladia.
Tarehe 12 Juni miaka 483 iliyopita nchi ya Chile iliyoko magharibi mwa Amerika ya Kusini ilitekwa na wakoloni wa Hispania. Kabla ya hapo Wahindi Wekundu wa Chile walikuwa wamevunja hujuma na mashambulio kadhaa ya Wahispania waliokusudia kuteka na kukalia kwa mabavu ardhi yao. Hata hivyo, hata baada ya kutekwa nchi yao, Wahindi Wekundu hao waliendeleza mapambano dhidi ya wakoloni hadi pale José Francisco de San Martín jenerali wa Argentina alipowasili mwaka 1817 na kuanzisha mashambulio ya kuzikomboa nchi zote zilizokuwa chini ya ukoloni wa Hispania Kusini mwa Amerika, ikiwemo Chile. Kwa msingi huo, Chile akakombolewa na kutangaza uhuru wake mwaka 1818. ***
Katika siku kkama ya leo miaka 110, kwa mara ya kwanza kabisa yalifanyika majaribio ya kutumia nishati ya joto la jua pambizoni mwa Cairo mji mkuu wa Misri. Mbunifu na mtekelezaji wa mpango huo alikuwa mwanafizikia wa Kijerumani, ambaye aliweza kukusanya miale ya jua na kufanikiwa kuwasha mashine ya mvuke yenye kutumia 'horse power' 50. ***
Miaka 110 iliyopita katika siku kama ya leo kwa mujibu wa kalenda ya Hijria, alizaliwa Sheikh Muhammad al-Ghazali, msomi, mwandishin na alimu mkubwa wa Kimisri. Muhammad al-Ghazali alizaliwa na kukulia katika familia iliyokuwa imeshikmana na dini. Kutokana na hima na idili kuubwa aliyokuwa katika masomo, Muhammad al-Ghazali alifanikiwa kuhitimuu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar akiwa na umri wa miaka 26 sambamba na kupata idhini ya kufundisha chuo hapo. Muhammad al-Ghazali ameandika vitabu visivyopungua 94. Msomii huyu alifanya hima na juhudi kubwa pia za kupigania umoja katika jami ya Kiislamu. Muhammad al-Ghazali aliaga dunia 20 Mfunguo Mosi Shawwal 1416 Hijria. ***
Siku kama ya leo miaka 84 iliyopita, alifariki dunia huko Najaf, Iraq Allamah Muhammad Hussein Kampani, mwanafalsafa, faqihi na mwanairfani mkubwa. Alizaliwa mwaka 1296 Hijria mjini Kadhimain nchini Iraq. Msomi huyo mkubwa alitabahari katika elimu za falsafa, tiba, irfan, historia, jiografia, mashairi na fasihi. Mbali na hayo Allamah Hussein Kampani alikuwa na fikra pevu na uwezo mkubwa wa kubainisha mambo. Msomi huyo ameandika vitabu kadhaa katika nyanja mbalimbali ikiwemo diwani ya mashairi akisifu viongozi wa Uislamu. ***
Siku kama ya leo miaka 44 iliyopita, inayosadifiana na 23 Khordad 1359 Hijria Shamsia, Imam Ruhullah Khomeini mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwa na lengo la kufanya mabadiliko katika vyuo vikuu hapa nchini, alitoa amri ya kuasisiwa Baraza Kuu la Mapinduzi la Kiutamaduni. Katika ujumbe wake, Imam Khomeini MA aliwataka wajumbe wa baraza hilo kuratibu na kuandaa mipango na mitalaa katika kozi mbalimbali za vyuo vikuu inayokwenda sambamba na mafunzo ya utamaduni tajiri wa Kiislamu. ******
Siku kama ya leo miaka 41 iliyopita, Bi. Nusrat Amin, faqihi na mfasiri mkubwa wa Qurani Tukufu alifariki dunia katika mji wa Isfahan ulioko katikati mwa Iran. Bi. Nusrat Amin aliutumia muda wake wote katika kuishughulikia Qurani Tukufu na kufanikiwa kufasiri kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu katika juzuu 15 na kuandika vitabu vingine vingi. Miongoni ma vitabu vya msomi huyu ni Al Sayr Wassuluuk, rahe Khoshbakhti na Nafahaat Rahmaniyya. ***