Oct 12, 2024 22:37 UTC
  • Jumapili, Oktoba 13, 2024

Leo ni Jumapili 9 Mfunguo Saba Rabiuthani 1446 Hijria mwafaka na 13 Oktoba 2024 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 2563 iliyopita mji wa kihistoria wa Babel ulitekwa na Kurosh, mwasisi wa utawala wa kizazi cha Hakhamaneshi nchini Iran. Ili kuweza kuudhibiti mji huo ambao ulikuwa na ngome kubwa na imara, Kurosh aliamuru kubadilishwa mkondo wa Mto Tigris uliokuwa ukipita katikati ya mji wa Babel. Kwa utaratibu huo askari wa Kurosh walitumia njia ya zamani ya maji ya mto huo kuingia na kisha kuuteka mji wa Babel. Mji huo ulioko kusini mwa eneo la Mesopotamia katika Iraq ya sasa, ulikuwa katika kilele cha maendeleo na nguvu kubwa katika kipindi hicho.

Hati ya haki za binadamu

 

Katika siku kama ya leo miaka 142 iliyopita alifariki dunia Ayatullah Haj Mirza Abdul Rahim Nahavandi, alimu na msomi mkubwa wa sheria za Kiislamu. Ayatullah Nahavandi alibobea katika elimu ya fiqhi na usulu fiqhi, na kutokana na hali hiyo wasomi wengi wa Iraq na Iran waliweza kustafidi na elimu yake. Inafaa kufahamisha kwamba, Ayatullah Haj Mirza Abdul Rahim Nahavandi, alizaliwa katika mji wa Nahavand, ulio magharibi mwa Iran na akiwa kijana alielekea mjini Najaf, Iraq na kusoma kwa walimu wakubwa wa zama hizo hususan Sheikh Murtadha Answari, ambapo kwa kipindi cha miaka 30 alijikita katika shughuli ya ufundishaji wa sheria za Kiislamu. ***

 

Miaka 142 iliyopita katika siku kama hii ya leo, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 58, Ayatullah Sayyid Haidar Hilli. Abul-Hassan Sayyid Haidar Bin Sulaiman bin Daud Hilli Husseini, ni miongoni mwa malenga na viongozi mashuhuri wa fani hiyo katika zama hizo. Ufasaha na uwezo mkubwa wa kiimani aliokuwa nao, vilimsukuma katika kuwasifu Ahlu Baiti wa Mtume (saw) kupitia mashairi yake. Miongoni mwa athari zake ni pamoja na kitabu cha 'ad-Duraru-Yatim' na 'al-Aqdul-Mufaswal.'