Jumamosi, 16 Novemba, 2024
Leo ni Jumamosi 14 Mfunguo Nane, Jamadul Awwal 1446 Hijria mwafaka na 16 Novemba 2024 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 381 iliyopita Jean Chardin mtambuzi wa masuala ya Mashariki na mwanafalsafa mtajika wa Ufaransa alizaliwa katika mji wa Paris. Alikulia na kusoma katika mji huo. Baba yake Jean Chardin alikuwa sonara na alijifunza tangu akiwa mtoto mdogo utambuzi wa mawe, madini na taaluma ya usonara.
Miaka 134 iliyopita katika siku kama ya leo Mulla Ismail Sabzavari, mpokezi wa hadithi na khatibu wa karne ya 13 Hijria aliaga dunia mjini Tehran. Alizaliwa Sabzevar moja ya miji ya kaskazini mashariki mwa Iran na kusoma falsafa kwa Mullah Hadi Sabzevari, mwanafalsafa mashuhuri wa Kiirani. Baadaye alielekea Najaf Iraq kwa ajili ya kujiendeleza zaidi katika Hawza mashuhuri ya mji huo. Alirejea baada ya kupata daraja ya Ijtihad. Mwanazuoni huyu amendika pia vitabu katiika taaluma mbalimbali.
Katika siku kama ya leo miaka 120 iliyopita, Abdul-Ghaffar Tehrani mwenye lakabu ya Najm al-Dawlah mwanahisabati wa Kiirani aliaga dunia. Alionyesha kipaji na mapenzi ya hali ya juu na elimu ya hisabati tangu alipokuwa shuleni. Alisoma elimu hiyo katika shule mashuhuurii za wakati huo kama Dar al-Funun. Baadaye Najm al-Dawlah alianza kufanya uhakiki katika hisabati. Moja ya vitabu vyake mashuhuri ni Bidayat al-Hisab.
Miaka 79 iliyopita katika siku kkama ya leo, vikosi vya jeshi la Ufaransa viliishambulia Vietnam na kuanza mapambano ya muda mrefu ya wananchi kwa ajili ya kuikomboa nchi hiyo. Baada ya karne moja ya kukoloniwa Vietnam na Ufaransa, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia Japan iliidhibiti nchi hiyo. Japan iliondoka Vietnam baada ya kushindwa katika vita hivyo, na Vietnam ikaanza kukaliwa kwa mabavu na Ufaransa.
Katika sikku kama ya leo miaka 56 iliyopita aliaga dunia Ustadh Ibrahim Pourdavud, mhakiki mkubwa na mtaalamu wa masuala ya Iran akiwa na umri wa miaka 83. Alielekea katika nchi za Ujerumani na India na kufundisha katika vyuo vikuu vya nchi hizo kwa ajili ya kukamilisha utafiti wake kuhusiana na masuala ya Iran. Mwaka 1315 Hijria Shamsia mhakiki huyo mkubwa aliitwa kufundisha katika Chuo Kikuu cha Tehran na mwaka 1346 alitunikiwa tuzo ya Sayansi ya Vatican kutokana na huduma zake kubwa za masuala ya kibinadamu. Msomi huyo ameandika vitabu kadhaa vikiwemo Utamaduni wa Iran ya Kale, Anahita na Hormuz-Nameh.
Siku kama ya leo miaka 45 iliyopita ulianzishwa tena uhusiano wa Iran na Libya. Uhusiano huo ulikatwa kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini. Sababu ya kukatwa uhusiano huo ni msimamo wa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi aliyeitambua serikali ya Shah nchini Iran kuwa ilikuwa tegemezi kwa ubeberu wa Marekani na kwamba ilitanguliza mbele maslahi ya nchi za Magharibi na utawala ghasibu wa Israel kuliko maslahi ya nchi za Kiarabu na Wapalestina.