Nov 30, 2024 02:34 UTC
  • Jumamosi, 30 Novemba, 2024

Leo ni Jumamosi 28 Mfunguo Nane Jamadul-Awwal 1446 Hijria ambayo inasadifiana na 30 Novemba 2024 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 357 iliyopita, Jonathan Swift mwandishi mashuhuri wa Ireland alizaliwa huko Dublin mji mkuu wa nchi hiyo. Swift alishiriki pakubwa katika harakati za ukombozi wa Ireland. Baadaye, Jonathan Swift alianza kujishughulisha na kazi ya uandishi. Swift alifariki dunia akiwa na miaka 78. ***

Jonathan Swift

 

Siku kama ya leo miaka 207 iliyopita, alizaliwa Theodor Mommsen mwanahistoria na mtafiti wa Ujerumani. Baada ya kumaliza masomo, Mommsen alijishughulisha na utafiti kuhusiana na vitabu tofauti na athari za tamaduni za zamani. Miongoni mwa vitabu vyake maarufu zaidi ni kitababu kinachoitwa 'Historia ya Roma ya Kale' ambacho ndiyo kitabu kamili cha historia ya mji wa Roma. Mwanahistoria huyo wa Ujerumani alitunukiwa tuzo ya Nobel katika fasihi hapo mwaka 1902 na alifariki dunia mwaka mmoja baadaye, akiwa na umri wa miaka 86.  **

Theodor Mommsen

 

Miaka 189 iliyopita katika siku kama ya leo, alizaliwa Mark Twain mwandishi mashuhuri wa Kimarekani. Twain alikipitisha kipindi cha utoto na ubarobaro wake na matukio yasiyo ya kawaida ambayo baadaye yalikuja kuwa maudhui kuu ya vitabu vyake. Mark Twain alikuwa mwandishi mwenye utani na mzaha. Aliandika visa na simulizi nyingi kwa ajili ya watoto na vijana wadogo ambapo tunaweza kuashiria hapa vitabu vyake viwili vya The Andventures of Tom Sawyer na (Matukio Yasiyo ya Kawaida ya Tom Sawyer) The Prince and The Pauper (Mrithi wa Kiti cha Ufalme na Ombaomba). Mwishoni mwa umri wake Mark Twain alikumbwa na ukata na umasikini mkubwa na hatimaye akaaga dunia mwaka 1910 baada ya kuugua.  

Mark Twain

 

Katika siku kama ya leo miaka 124 iliyopita, aliaga dunia Oscar Wilde, mwandishi na malenga mahiri wa Ireland. Wilde alizaliwa mwaka 1854 katika familia iliyokuwa na mapenzi maalumu na masuala ya kiutamaduni na Sanaa. Baada ya kukamilisha masomo yake ya sekondari alijiunga na Chuo Kikuu. Oscar Wilde alianza kujihusisha na taaluma ya uandishi akiwa katika rika la ujana na katika kipindi kifupi cha umri wake alifanikiwa kuandika vitabu mbalimbali vilivyokuwa na madhumuni ya riwaya, mashairi na maigizo. Baadhi ya vitabu vya Oscar Wilde ni The Model Millionaire, The Soul of Man Under Socialism na The Canterville Ghost. 

Oscar Wilde

 

Siku kama hii ya leo miaka 86 iliyopita Ayatullah Sayyid Hassan Mudarres, mwanazuoni mwanamapambano na mpigania ukombozi wa Kiirani aliuawa shahidi na vibaraka wa Reza Khan, mtawala dhalimu wa Iran wa wakati huo katika mji wa Kashmar kaskazini mashariki mwa Iran. Ayatullah Sayyid Hassan Mudarres aliamua kuanzisha mapambano dhidi ya utawala huo baada ya kujionea dhulma na ukandamizaji wa mtawala Reza Khan nchini Iran. Alifanya jitihada kubwa za kutekelezwa sheria za Kiislamu hapa nchini na kuiokoa Iran kutoka kwenye makucha na udhibiti wa wakoloni. Kwa msingi huo mtawala kibaraka wa wakati huo wa Iran, Reza Khan Pahlavi alimuona kuwa adui mkubwa na kuchukua uamuzi wa kumuua. 

Ayatullah Sayyid Hassan Mudarres

 

Miaka 36 iliyopita katika siku kama ya leo, aliaga dunia Ustadh Abdul-Basit Abdul-Samad katika mji wa Cairo nchini Misri. Abdul Basit alikuwa mmoja wa waalimu na maqarii wakubwa wa Qur'ani Tukufu. Alianza kujifunza Qurani Tukufu akiwa mdogo na alipofikia umri wa miaka 12 akafanikiwa kupata tuzo ya kuhifadhi na kusoma Qur'ani. Katika maisha yake Ustadh Abdul-Basit alijishughulisha na usomaji wa Qurani Tukufu na kutunukiwa zawadi na tunzo muhimu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani tukufu kwenye nchi mbalimbali za Kiislamu, sambamba na kuwavutia Waislamu wengi kwenye kusoma maneno hayo ya Mwenyezi Mungu. Abdul Basit ameacha kanda nyingi za sauti yake nzuri ya qiraa ya Qur'ani Tukufu. 

Ustadh Abdul-Basit Abdul-Samad