Jan 10, 2025 02:24 UTC
  • Ijumaa, 10 Januari, 2025

Leo ni Ijumaa tarehe 9 Rajab 1446 Hijria sawa na Januari 10 mwaka 2025.

Siku kama hii ya leo miaka 483 iliyopita aliuawa shahidi Izuddin Sayyid Hussein, mmoja wa wasomi wakubwa wa Kiislamu wa karne ya 10 Hijria. 

Alizaliwa mwaka wa 906 Hijria katika mojawapo ya vijiji vya Jabal Amil huko Lebanon na kujifunza elimu za wakati huo. 

Watu wenye chuki na husda, ambao hawakuweza kuvumilia utu na shakhsia yake kubwa ya kiroho na kidini katika mji wa Sayda (Sidon) huko Lebanon, walimpa sumu mwanazuoni huyo mkubwa wa Kiislamu na kumuua katika siku kama hii ya leo.

Katika siku kama ya leo miaka 201 iliyopita inayosadifiana na 10 Januari 1824, Joseph Aspdin mwanakemia wa Uingereza alifanikiwa kutengeneza saruji na kwa utaratibu huo kulipatikana mabadiliko makubwa katika shughuli za ujenzi. 

Hatua hiyo ilitambuliwa kama tukio kubwa katika shughuli za kimaendeleo na ujenzi mpya wa nyumba. Joseph Aspdin ambaye alikuwa akifanya utafiti kwa miaka kadhaa ili kutengeneza mada ambayo ingesaidia kuimarisha msingi wa nyumba, hatimaye alifanikiwa kutengeneza saruji baada ya majaribio chungu nzima.  ***

Siku kama ya leo miaka 105 iliyopita, inayosadifiana na 10 Januari 1920, Jumuiya ya Mataifa ilianza shughuli zake rasmi huko Geneva, Uswisi.

Jumuiya hiyo iliundwa baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia kwa shabaha ya kuimarisha amani na usalama duniani. Mwanzoni nchi za Kiafrika na Urusi hazikujiunga na jumuiya hiyo na badala yake nchi za Uingereza na Ufaransa ndizo zilizobeba jukumu la kuzisaidia nchi hizo.

Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, mnamo mwezi Aprili 1946, uliundwa Umoja wa Mataifa na kuchukua nafasi ya Jumuiya ya Mataifa, ingawa matatizo yaliyokuwa yakiikumba Jumuiya ya Mataifa bado yanaendelea kuukumba Umoja wa Mataifa hadi hii leo.

Siku kama ya leo miaka 62 iliyopita, wataalamu wawili wa Uswisi walifanikiwa kutengeneza saa ya elekroniki.

Baada ya miaka 12 ya juhudi kubwa, hatimaye wataalamu Solvil na Titus walifanikiwa kutengeneza chombo hicho kwa kuweka vifaa kadhaa muhimu na makini. Aina hii ya saa ni makini mno na hufanya makosa machache sana ikilinganishwa na saa nyingine. 

Siku kama ya leo miaka 68 iliyopita aliaga dunia Ustadh Abulqassim Sahab, mmoja wa wasomi wakubwa wa elimu ya jiografia na mtafiti mashuhuri wa Kiirani. Alizaliwa mwaka 1266 Hijria Shamsiya katika mji wa Tafresh nchini Iran. Abulqassim Sahab alijifunza fiqih na usul kwa maulamaa wa mji huo na mbali na kupata elimu hiyo alizungumza pia lugha za Kiingereza na Kijerumani. 

Abulqassim Sahab

Miaka 13 iliyopita katika siku kama hii ya leo msomi wa nyuklia wa Iran, Mustafa Ahmad Roshan aliuawa shahidi na maajenti wa utawala haramu wa Israel.

Ahmad Roshan alikuwa msomi wa nne wa nyuklia wa Iran kuuawa na magaidi wa Israel na washirika wake. Mbali na kujishughulisha na masuala ya nyuklia msomi huyo alifanya utafiti mkubwa katika masuala ya elimu na sayansi. Ahmad Roshan aliuawa yeye na dereva wake mjini Tehran akiwa njiani kueleka kazini kwake.

Siku kadhaa baadaye genge la magaidi waliomuua msomi huyo wa nyuklia wa Iran na wenzake lilitiwa nguvuni na wanachama wake wakakiri kuwa wana uhusiano na utawala haramu wa Israel na kwamba walipewa mafunzo na maajenti wa utawala huo haramu kwa ajili ya kuwaua kigaidi wasomi wa nyuklia wa Iran.