Jun 15, 2026 04:06 UTC
  • Jumatatu, 15 Juni, 2026

Leo ni Jumatatu 29 Mfunguo Tatu Dhul-Hija 1447 Hijria sawa na 15 Juni 2026.

Tarehe 15 Juni miaka 318 iliyopita katika siku kama ya leo harakati ya wapigania uhuru wa Scotland ilikandamizwa vikali na Uingereza.

Uingereza daima imekuwa ikifanya jitihada za kuiunganisha Scotland na ardhi ya kaskazini mwa nchi hiyo. Hata hivyo harakati za mapambano za Wascotland zilipinga vikali suala hilo.

Hata hivyo mwaka 1707 mabunge ya nchi hizo mbili yaliunganishwa. Suala hilo liliwakasirisha sana Wascotland walioanzisha harakati nyingine ya mapambano mbayo ilikandamizwa vikali katika siku kama ya leo hapo mwaka 1708. ***

Siku kama ya leo miaka 178 iliyopita sawa na tarehe 15 Juni 1848, Otto von Bismarck Kansela wa Ujerumani aliuchagua mji wa kihistoria na maarufu wa Berlin, kuwa mji mkuu wa nchi hiyo.

Kuteuliwa mji wa Berlin kuwa mji mkuu wa Ujerumani, kulitokana na utekelezaji wa mpango wa kuziunganisha Ujerumani mbili, uliobuniwa na Kansela Bismarck.

Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Ujerumani iligawanyika katika sehemu mbili za Mashariki na Magharibi. Mwezi Septemba 1990 baada ya kuvunjwa ukuta wa Berlin, kuliandaliwa mazingira ya kuunganishwa pande hizo mbili, na hatimaye Berlin kurejea tena na kuwa mji mkuu wa Ujerumani.  ***

Miaka 109 iliyopita katika siku kama hii ya leo inayosadifiana na tarehe 29 Dhulhija aliuawa shahidi Sheikh Muhammad Khiyabani, mwanamapambano katika kipindi cha kupigania katiba, na kukandamizwa harakati ya msomi huyo na wafuasi wake katika mji wa Tabriz, ulioko Kaskazini Magharibi mwa Iran.

Baada ya kujipatia elimu kwa maulamaa wakubwa, Sheikh Khiyabani alianza harakati za kupinga dhulma na ukandamizaji zilizokuwa zikifanywa na tawala za silsila ya Qajar hapa nchini. Baada ya kuusambaratisha udikteta wa Muhammad Ali Shah Qajar na kumlazimisha mtawala huyo kukimbia nchin mwaka 1287 Hijria Shamsia, wananchi wa Tabriz walimchagua Sheikh Muhammad Khiyabani kuwa mwakilishi wao katika Bunge la Taifa la Iran.

Hata hivyo katika siku kama ya leo Sheikh Khiyabani alikamatwa na kuuawa shahidi, wakati alipokuwa akipambana na askari wa utawala wa kifalme.    ****

Katika siku kama ya leo miaka 98 iliyopita, Fazliddin Mohammadiev, mwandishi wa vitabu na mwandishi wa habari maarufu wa Tajikistan, alizaliwa huko Samarkand.

Alianza kazi yake kama mwandishi wa gazeti la "Red Tajikistan" na baada ya kusoma katika Shule ya Kati ya Komsomol huko Moscow, alifikia nyadhifa muhimu katika magazeti ya Tajikistan na Kamati ya Sinema ya Tajikistan. Mohammadiev alikuwa mwandishi ambaye alionyesha maendeleo ya kijamii ya Tajikistan kwa kuzingatia.

Kazi zake ni pamoja na hadithi fupi, riwaya fupi na riwaya ambazo mara nyingi huandikwa kwa nathari rahisi na safi na michezo ya kuchekesha.     *****

Miaka 24 iliyopita katika siku kama ya leo, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ilianzishwa baada ya kusainiwa makubaliano kati ya nchi za Urusi, Uchina, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Uzbekistan.

Lengo la kuanzishwa jumuiya hiyo lilikuwa ni kuongeza ushirikiano wa kiuchumi, kiutamaduni na usalama.

Historia ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai inaanzia 1996, wakati nchi hizi, isipokuwa Uzbekistan, zilipoanzisha kile kinachoitwa mkataba wa "Shanghai 5" ili kuimarisha uaminifu na kuongeza usalama katika mipaka yao mirefu.

Kwa kujiunga Uzibekistan na Shanghai 5, kundi hilo lliligeuka na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Hii leo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, India, Pakistan, Afghanistan na Mongolia pia ni wanachama wa jumuiya hiyo.    ****