Dec 15, 2022 22:55 UTC
  • Ijumaa tarehe 16 Disemba 2022

Leo ni tarehe 21 Jumadil Awwal 1444 Hijria sawa na tarehe 16 Disemba 2022.

Miaka 1123 iliyopita katika siku kama ya leo sawa na tarehe 21 Mfunguo 8 mwaka 320 Hijria, alizaliwa Abu Jaafar Ahmad bin Ibrahim Qirawani, aliyekuwa mashuhuri kwa jina la Ibn Jazzar. Msomi huyo wa Morocco alikuwa tabibu, mwanafalsafa na mwanajiografia mashuhuri wa Kiislamu. Ibn Jazzar alikuwa tabibu mwenye moyo wa kujitolea na anayewatakia watu kheri na aliandika kitabu alichokipa jina la "Twibul Fuqaraa” au Tiba ya Watu Maskini." Mwanafalsafa huyo ameandika vitabu 20. Miongoni mwa vitabu vyake ni Risalatun Fii Ibdalil Adwiya na Zadul Musafir.

Ibn Jazzar

Siku kama hii ya leo miaka 31 iliyopita Kazakhstan ilijitangazia uhuru baada ya kudhihiri dalili za kusambaratika Urusi ya zamani. Wakazaki ambao wanaunda jamii kubwa zaidi nchini humo na ambao ni kutoka makabila ya Waturki na Wamongoli, katika karne ya 17 miladia, waligawanyika katika sehemu tatu za tawala kubwa za kisultani. Mwanzoni mwa karne ya 18 taratibu waliwekwa chini ya udhibiti wa Warusi na wakati huo khususan katika karne ya 19 Miladia, Wakazaki hao wakiwa pamoja na watu wa maeneo mengine ya Asia ya kati walijiunga na dini ya Kiislamu.

Bendera ya Kkazakhstan

Katika siku kama ya leo miaka 25 iliyopita kanali ya televisheni ya Sahar ya Kitengo cha Matangazo ya Ng'ambo cha Shirika la Redio na Televisheni la Iran ilianza kazi zake kwa kurusha matangazo ya lugha za Kiarabu, Kiazari, Kibosnia, Kituruki, Kifaransa, Kiingereza na Kiurdu. Televisheni za kanali hiyo zinatayarisha na kurusha matangazo mbalimbali yanayolenga familia katika masuala ya kijamii, kisiasa, filamu, sinema za matukio ya kweli, masuala ya kiuchumi na kadhalika. Vilevile televisheni hizo huakisi habari za matukio mbalimbali ya kieneo na kimataifa.

Siku kama hii ya leo miaka 24 iliyopita Mahakama ya Rufaa ya Paris ilimhukumu kifungo na kumtoza faini mwanafalsafa na msomi mashuhuri wa nchi hiyo, Roger Garaudy, kwa kosa eti la kukana jinai dhidi ya binadamu katika kitabu chake cha 'The Founding Myths of Israeli Politics'. Katika kitabu hicho msomi huyo Mfaransa alithibitisha kisayansi na kwa hoja madhubuti kwamba Wazayuni walishirikiana na Manazi katika Vita vya Pili vya Dunia. Vilevile amethibitisha kwa hoja na ushahidi kwamba, kwa shabaha ya kutaka kupata uungaji mkono wa kuunda dola bandia la Israel katika ardhi ya Palestina, Wazayuni walikuza na kutia chumvi kupita kiasi jinai zilizofanywa na Adolph Hitler dhidi ya Mayahudi. Katika kitabu cha 'The Founding Myths of Israeli Politics' Profesa Garaudy anasema, idadi ya Mayahudi milioni 6 inayotajwa na Wazayuni kuwa iliuawa na Wajerumani wa zama za Hitler imetiwa chumvi kupita kiasi kwani jamii ya Wayahudi katika kipindi hicho haikuwa kubwa kiasi hicho. Msomi huyo alikamatwa na kuhukumiwa kifungo nchini Ufaransa kutokana na maoni yake, suala ambalo limethibitisha urongo wa madai ya demokrasia na uhuru wa maoni nchini Ufaransa.

Roger Garaudy,