Feb 19, 2018 15:28
Assalaamu Alaykum wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika kipindi hiki maalumu nilichokuandalieni kwa mnasaba wa kukumbuka siku aliyokufa shahidi Bibi Fatima Zahra (a.s) binti mtukufu wa Bwana Mtume (s.a.w) na mwanamke bora duniani na akhera, mwanamke ambaye ni kigezo na ruwaza njema. Amani iwe juu yako Ewe Fatma Zahra mwanamke bora wa duniani na Akhera, Bibi wa wanawake wa peponi, Mtukufu as-Sidiqah at-Tahirah Fatimatuz Zahra (Salaamullahi Alayha).