-
Operesheni kali dhidi ya mabaki ya wanachama wa Daesh (ISIS) yaanza nchini Iraq
May 05, 2020 11:20Msemaji wa Kamandi Kuu ya Jeshi la Iraq ameelezea amri ya Adil Abdul-Mahdi, Waziri Mkuu wa Iraq ya kuanzishwa operesheni kali dhidi ya mabaki ya wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) nchini humo.
-
Helikopta za Marekani zanaswa zikiwasafirisha magaidi wa DAESH (ISIS) kutoka Syria na kuwapeleka Iraq
May 04, 2020 14:09Harakati ya muqawama wa Kiislamu ya An-Nujabaa ya Iraq imetoa mkanda wa vidio unaoonyesha jinsi helikopta za jeshi la Marekani zinavyowahamisha kutoka Syria na kuwapeleka Iraq magaidi wa kundi la ukufurishaji la DAESH (ISIS).
-
Sababu za kudhihiri tena Daesh nchini Iraq
May 04, 2020 09:54Magaidi wa kundi la Daesh wameshambulia Harakati ya Wananchi wa Iraq Hashdu Sha'bi, na kuua pamoja na kujeruhi makumi ya wanaharakati wa kundi hilo la mapambano ya Kiislamu.
-
Hizbullah ya Iraq: Harakati za genge la Daesh (ISIS) zinatokana na mipango ya Marekani na Saudia
May 04, 2020 07:15Msemaji wa Kisiasa wa Kundi la Muqawama la Hizbullah ya Iraq amesema kuwa, harakati mpya za kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) katika mikoa tofauti ya nchi hiyo, zinahusiana na mipango ya Marekani na Saudi Arabia.
-
Wairaqi waandamana kulaana shambulizi la Daesh dhidi ya Hashd al-Sha'abi
May 03, 2020 08:09Wananchi wa Iraq wamefanya maandamano katika mji mkuu Baghdad kulaani shambulizi la hivi karibuni la kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) lililoua na kujeruhi makumi ya wanachama wa harakati ya kujitolea wananchi ya Hashdu Sha'abi.
-
Al-Hashd al-Shaabi: Magaidi wa ISIS Iraq ni chombo cha Marekani
Apr 25, 2020 04:05Mkuu wa Idara ya Mawasiliano katika Harakati ya Al-Hashd Al-Shaabi katika mkoa wa Diyala mashariki mwa Iraq amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh nchini hum ni chombo cha mashirika ya kijasusi ya Marekani.
-
Marekani ndiyo ilipanga mashambulizi ya hivi karibuni ya Daesh nchini Iraq
Apr 21, 2020 11:47Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa katika Bunge la Iraq amesema kuwa Wamarekani ndio waliopanga mashambulizi ya hivi karibuni ya magaidi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) nchini humo.
-
Yaelezwa kuwa kinara mpya wa Daesh (ISIS) amepenya nchini Iraq kwa msaada wa Marekani
Apr 20, 2020 17:25Chanzo kimoja cha usalama nchini Iraq kimesema kuwa, kwa mujibu wa taarifa za kiintelejensia zilizopatikana, Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurashi, kiongozi mpya wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) amepenya nchini humo kwa msaada wa askari magaidi wa Marekani.
-
Kukiri Masoud Barzani; Iran na shahidi Soleimani ndio waliongoza mapambano dhidi ya Daesh
Apr 11, 2020 10:09Masoud Barzani, Mkuu wa chama cha Demokrasia cha Kurdistan huko Iraq amefanya mahojiano na televisheni ya MBC ya nchini Saudi Arabia na kukiri kuwa Iran na Luteni Jenerali shahidi Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH walikuwa wa awali kabisa kulisaidia eneo la Kurdistan ya Iraq kuendesha vita dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh.
-
Rezai: Hatua yoyote ya kijeshi itakayochukua Marekani Iraq ni sawa na shambulio linalofanywa na DAESH (ISIS)
Mar 31, 2020 15:53Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema, hatua yoyote ya kijeshi itakayochukua Marekani nchini Iraq itakuwa sawa na hujuma inayofanywa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS).