-
Hashdu Sha'abi yatekeleza operesheni ya mafanikio katika mikoa minne ya Iraq
Mar 01, 2020 02:41Kamandi ya Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi ya Iraq imetangaza kumalizika kwa operesheni ya mafanikio makubwa dhidi ya magaidi katika mikoa minne ya Al-Anbar, Diyala, Kirkuk na Salahdin.
-
Hatua ya kukurupuka ya Marekani ya kumuwekea vikwazo Katibu Mkuu wa Kataeb Hizbullah ya Iraq
Feb 28, 2020 05:35Marekani imetuma idadi kubwa ya wanajeshi wake huko Iraq tangu mwaka 2014 kwa kisingizio cha kupambana na kundi la Daesh. Katika hatua yake ya kukurupuka Marekani imeliorodhesha jina la kiongozi wa mojawapo ya makundi muhimu ya taasisi ya Kataeb Hizbullah ya Iraq licha ya nafasi muhimu ya kundi la kujitolea la wananchi la al Hashd al Shaabi katika kutoa pigo na kuliangamiza kundi la kigaidi la Daesh huko Iraq.
-
Misri yawahukumu watu kadhaa kifungo cha maisha jela kwa kujiunga na Daesh
Jan 28, 2020 08:11Mahakama Cairo nchini Misri imewahukumu watu wasiopungua 37 vifungo mbalimbali vya jela kikiwemo kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kujiunga na kuliunga mkono genge la uhalifu lenye mfungamano na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.
-
Ujerumani yatahadharisha kuhusu kuanza tena mashambulizi ya kundi la Daesh
Jan 25, 2020 03:13Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ametahadharisha kuwa, kuna uwezekano kundi la kigaidi la Daesh likaanza tena kutekeleza vitendo vyake vya kigaidi.
-
"ISIS walitaka kushambulia ubalozi wa Marekani Lebanon na kuisingizia Hizbullah"
Jan 24, 2020 06:15Gazeti la al Jamhuriyyah la Lebanon limefichua kuwa, genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) lilikuwa limepanga njama za kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Beirut ili kuibebesha lawama harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Hizbullah hasa baada ya Marekani kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.
-
Mufti 'tipwatipwa' wa DAESH mwenye uzito wa kilo 245 atiwa nguvuni mjini Mosul, Iraq
Jan 18, 2020 14:07Vikosi vya usalama vya Iraq vimemtia nguvuni Abu Abdul Bari, mufti wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH (ISIS) katika mji wa Mosul, kaskazini mwa nchi hiyo. Abu Abdul Bari ni maarufu kwa utoaji fatua za kuwafanya wanawake watumwa, za ubakaji, utesaji na uangamizaji wa kimbari.
-
TV ya Saudia yamtimua mtangazaji wa Palestina kwa kutangaza mshikamano na Wayemen
Jan 14, 2020 04:30Televisheni ya Saudi Arabia imemsimamisha kazi mtangazaji wake baada ya kubainika kwamba, amekuwa akituma ujumbe katika mtandao wa kijamii wa Twitter akitangza mshikamano wake na Wayemen na kulaani mashambulizi yanayofanywa na utawala wa Riyadh dhidi ya raia wasio na hatia wa Yemen.
-
Ngome kubwa ya ISIS yaharibiwa kaskazini mwa Iraq
Jan 12, 2020 12:13Vikosi vya Kujitolea vya Wananchi wa Iraq maarufu kama Al Hashd al Shaabi vimeharibu pango kubwa zaidi la magaidi wa ISIS (Daesh) kaskazini mwa Iraq.
-
Watu 30 wauawa katika mripuko wa bomu nchini Nigeria
Jan 07, 2020 08:06Kwa akali watu 30 wameuawa huku makumi ya wengine wakijeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea karibu na daraja lenye shughuli nyingi katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran; Ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani
Jan 06, 2020 02:40Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kuwa ulimwengu mzima una wajibu wa kukabiliana na hatua ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Kamanda Qassem Soleimani; na watu wote wanapaswa kutekeleza majukumu yao mbele ya jinai hiyo.