Ujerumani yatahadharisha kuhusu kuanza tena mashambulizi ya kundi la Daesh
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ametahadharisha kuwa, kuna uwezekano kundi la kigaidi la Daesh likaanza tena kutekeleza vitendo vyake vya kigaidi.
Bi Annegret Kramp- Karrenbauer amesema pambizoni mwa Mkutano wa Kiuchumi wa Davos kuwa kuna hatari kundi la kigaidi la daesh likaanza tena harakati za kigaidi iwapo mashinikizo dhidi ya kundi hilo yatapungua.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani pia ametetea kuendelea kuwepo wanajeshi wa nchi yake huko Iraq.
Ujerumani ina wanajeshi 120 katika ardhi ya Iraq lakini wamesitisha oparesheni zao za kijeshi nchini humo. Wanajeshi hao zaidi wanajishughulisha na masuala ya kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Iraq.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ameeleza wasiwasi wake kuhusu uwezekano wa kuanza tena hujuma za kundi la kigaidi la Daesh katika hali ambayo ikulu ya Rais wa Marekani (White House) na nchi za Ulaya washirika wa Washington, katika miaka ya karibuni zimekuwa wafadhili wakubwa wa makundi ya kigaidi huko Iraq na Syria.