-
Mtandao mkubwa wa kimataifa unaolifadhili kifedha DAESH Iraq wasambaratishwa
Feb 21, 2019 15:36Shirika la Intelijensia la Iraq limeeleza katika taarifa maalumu iliyotolewa leo, kwamba limeugundua na kuusambaratisha "mtandao mkubwa zaidi wa ufadhili wa kifedha" kwa ugaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.
-
Trump: Mwanamke mwanachama wa DAESH (ISIS) hana ruhusa ya kuingia Marekani
Feb 21, 2019 15:31Rais Donald Trump wa Marekani amesema, Hoda Muthana, mwanamke ambaye ni mwanachama wa kundi la kigaidi la DAESH (ISIS), hana ruhusa ya kuingia nchini humo. Trump ametoa agizo hilo pasi na kuashiria hatua zilizochukuliwa na serikali ya Washington katika kuanzisha na kuliunga mkono kundi hilo la ukufurishaji.
-
Mamia ya wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) wajisalimisha kwa jeshi la Syria
Feb 21, 2019 07:41Idadi kubwa ya wachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) wamejisalimisha kwa jeshi la serikali ya Syria kutokana na kukaribia kuibuka mapigano makali kati ya magaidi hao na wapiganaji wa Kikurdi wanaoitwa 'Syrian Democratic Forces' katika eneo la Al-Baghuz, mashariki mwa nchi hiyo.
-
Madai ya kichekesho ya Pompeo kuhusu kundi la kigaidi la Daesh
Feb 21, 2019 02:54Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ametoa madai ya kichekesho akisema kuwa nchi yake itabadili mbinu za kukabiliana na kundi la kigaidi la Daesh.
-
Mkuu wa al Hashdu al Sha'abi: Iran imeisaidia Iraq katika mapambano dhidi ya Daesh
Feb 18, 2019 02:32Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya al Hashdu al Sha'abi na Baraza la Usalama wa Taifa la Iraq amesema kuwa Iran ni nchi pekee ambayo iliisaidia Iraq katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh.
-
Kamanda wa jeshi la Marekani akiri kwamba nchi hiyo imeshindwa huko Syria
Feb 16, 2019 01:26Kamanda wa kikosi maalumu cha jeshi la Marekani amekiri kwamba uingiliaji kijeshi wa nchi hiyo dhidi ya Syria haukuwa na mafanikio.
-
Safari ya kushtukiza ya Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Marekani nchini Iraq
Feb 13, 2019 13:00Baada ya baadhi ya maeneo ya Iraq kudhibitiwa na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) mnamo mwezi Juni 2014, Marekani iliimarisha uwepo wake ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu sambamba na kuweka askari wake katika kambi kadhaa za kijeshi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.
-
CNN: Saudi Arabia imetuma silaha za Marekani kwa kundi la al Qaida huko Yemen
Feb 05, 2019 07:39Televisheni ya CNN ya Marekani imefichua kuwa silaha zilizotumwa na nchi hiyo kwa muungano wa Saudi Arabia na Imarati huko Yemen zimekabidhiwa kwa makundi ya kigaidi hususan al Qaida.
-
Al Hashdu sh-Sha'abi: Mashambulizi yetu dhidi ya Daesh huko Syria yameua na kujeruhi magaidi 35
Jan 19, 2019 07:38Kamanda wa Operesheni za mkoa wa Al Anbar za Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi nchini Iraq amesema kuwa, katika mashambulizi ya jana ya harakati hiyo dhidi ya ngome za magaidi wa kundi la Daesh (ISIS), magaidi 35 wa genge hilo wameuawa na kujeruhiwa.
-
Al Hashdu sh-Sha'abi yashambulia ngome za magaidi wa Daesh Deir ez-Zor, Syria
Jan 19, 2019 03:01Harakati ya Wananchi ya al Hashdu sh-Sha'abi nchini Iraq imefanya shambulizi dhidi ya ngome na maeneo ya magaidi wa kundi la Daesh (ISIS) katika mkoa wa Deir ez-Zor nchini Syria, ambapo kwa akali magaidi 15 wameangamizwa.