Madai ya kichekesho ya Pompeo kuhusu kundi la kigaidi la Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/world-i51687-madai_ya_kichekesho_ya_pompeo_kuhusu_kundi_la_kigaidi_la_daesh
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ametoa madai ya kichekesho akisema kuwa nchi yake itabadili mbinu za kukabiliana na kundi la kigaidi la Daesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 20, 2019 23:24 UTC
  • Madai ya kichekesho ya Pompeo kuhusu kundi  la kigaidi la Daesh

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ametoa madai ya kichekesho akisema kuwa nchi yake itabadili mbinu za kukabiliana na kundi la kigaidi la Daesh.

Akizungumza na kanali ya RUV ya televisheni ya serikali ya Iceland Mike Pompeo bila ya kuashiria nafasi ya ikulu ya Marekani (White House) katika kulianzisha kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh kwa ajili ya kuzusha machafuko katika eneo la Mashariki ya Kati, amedai kuwa Washington itaendelea kukabiliana na kundi hilo. Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ameongeza kuwa nchi yake itabadili mbinu za kukabiliana na Daesh.  

Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani 

Katika mahojiano hayo, Pompeo aidha amedhihirisha msimamo wa uhasama wa White House dhidi ya Iran ambapo kwa mara nyingine tena ameungumzia suala la Iran kuiunga mkono kambi ya muqawama. Pompeo ametoa madai hayo yote katika hali ambayo White House siku zote ndiyo muungaji mkono mkuu wa makundi ya kigaidi huko Iraq na Syria. Viongozi wa kijeshi wa Marekani aidha wamekiri kuwa nchi hiyo inawapatia misaada ya kifedha na kilojistiki makundi mbalimbali ya kigaidi.