-
Politico: Trump amewaambia viongozi wa nchi za Kiislamu hatairuhusu Israel iutwae Ukingo wa Magharibi
Sep 25, 2025 06:41Tovuti ya habari ya Politico imeripoti kuwa, katika mkutano wa faragha aliofanya Rais wa Marekani Donald Trump na viongozi wa nchi kadhaa za Kiarabu na Kiislamu, rais huyo wa Marekani aliwaahidi viongozi hao kwamba, hatamruhusu waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu autwae kikamilifu Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
-
Russia yajibu mapigo kwa Trump baada ya kuiita 'chui wa karatasi', yasema chaguo pekee ni vita
Sep 25, 2025 04:12Ikulu ya Kremlin imetangaza kuwa Russia haina "mbadala" isipokuwa kuendelea kupigana vita, huku ikijibu mapigo kwa mabadiliko ya ghafla yaliyoonyeshwa dhidi ya nchi hiyo na Rais wa Marekani Donald Trump mkabala wa Ukraine kwa kufikia hadi ya kuiita Moscow "chui wa karatasi".
-
Trump azishambulia China na India kwa kuziita 'wafadhili wakuu' wa vita vya Ukraine
Sep 25, 2025 04:12Rais wa Marekani Donald Trump amezituhumu India na China kuwa "zinafadhili kifedha" vita vya Ukraine kupitia uagizaji wa nishati kutoka Russia. Trump ametoa shutuma hizo katika hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini New York.
-
Kwa nini Waziri Mkuu wa India amewataka wananchi kutumia bidhaa za ndani?
Sep 24, 2025 11:08Waziri Mkuu wa India amewataka wananchi wa nchi hiyo kuacha kutumia bidhaa kutoka nje na badala yake watumie bidhaa za ndani kufuatia kushtadi mivutano katika uhusiano wa nchi hiyo na Marekani.
-
White House: Trump atakutana na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kujadili kadhia ya Ghaza
Sep 23, 2025 06:57Msemaji wa ikulu ya White House Karoline Leavitt ametangaza kuwa rais wa Marekani Donald Trump anatazamiwa kufanya mkutano na viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kujadili kadhia ya Ghaza.
-
Trump atoa vitisho dhidi ya Afghanistan endapo Taliban haitaikabidhi US kituo cha anga cha Bagram
Sep 21, 2025 03:24Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuchukua hatua kali ambazo hakuzitaja iwapo serikali ya Taliban nchini Afghanistan itakataa kukabidhi kituo cha jeshi la anga cha Bagram, ambacho kilitelekezwa wakati majeshi ya Marekani. yalipoondoka kifedheha katika ardhi ya nchi hiyo.
-
Duru za Uturuki: Erdogan amefanya mazungumzo ya siri Istanbul na mwana wa kiume wa Trump
Sep 19, 2025 11:07Mwana mkubwa wa kiume wa Rais Donald Trump wa Marekani na ujumbe alioandamana nao wiki iliyopita walikutana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mjini Istanbul wiki katika ziara ambayo haikutangazwa. Hayo yameripotiwa na duru zilizodai kuwa na uelewa wa suala hilo.
-
Taliban yamjibu Trump: Tunaweza kuzungumza, lakini Marekani haitaruhusiwa kuwepo tena kijeshi Afghanistan
Sep 19, 2025 11:05Serikali ya Afghanistan inayoongozwa na Taliban imetupilia mbali wito wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kutaka jeshi la nchi hiyo lirejee Afghanista na kupatiwa tena kambi ya jeshi la anga ya Bagram.
-
Uingereza inamngojea Trump amalize ziara yake ndipo itangaze kulitambua Dola la Palestina
Sep 18, 2025 10:12Uingereza itaitambua rasmi Palestina kama Dola mwishoni mwa wiki hii baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhitimisha ziara yake ya kiserikali nchini humo. Hayo yamefichuliwa na gazeti la The i Paper likivinukuu vyanzo vya serikali.
-
Maelfu waandamana London kupinga ziara ya Trump nchini Uingereza
Sep 18, 2025 07:22Maelfu ya wakazi wa jiji la London wameandamana kupinga ziara ya kiserikali ya Rais Donald Trump wa Marekani nchini Uingereza na kumtaja kama kiongozi mbaguzi na mpenda mabavu. Wafanya maandamano wamelaani pia sera za nje za Marekani kuhusu Iran na Gaza.