-
Makumi ya maiti zapatikana kwenye mto ulioko mpakani mwa eneo la Ethiopia la Tigray na Sudan
Aug 03, 2021 07:45Maiti zisizopungua 30 zilizosombwa na maji zimepatikana kwenye kingo za mto unaotenganisha Sudan na eneo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray. Hayo ni kwa mujibu wa wakimbizi wawili wa Ethiopia na mashuhuda wanne raia wa Sudan waliookota maiti hizo.
-
Umoja wa Mataifa: Tuna wasiwasi baada ya misaada ya kibinadamu kuchelewa kufika Tigray Ethiopia
Jul 31, 2021 22:00Umoja wa Mataifa Uujmetangaza kuwa, una wasiwasi kufuatia ucheleweshaji katika kupeleka misaada ya kibinadamu jimboni Tigray, kwa minajili ya kukabiliana na hali mbaya inayolikumba jimbo hilo la kaskazini mwa Ethiopia.
-
Mamia ya raia wauawa katika eneo la Somali nchini Ethiopia
Jul 27, 2021 10:57Serikali ya jimbo la Somali huko mashariki mwa Ethiopia imewatuhumu waasi kutoka jimbo jirani la Afar kuwa wameua mamia ya raia katika shambulio la hivi karibuni.
-
Wapiganaji wa eneo la Tigray Ethiopia watishia kuelekea Addis Ababa
Jul 25, 2021 06:53Harakati ya Ukombozi ya eneo la Tigray (TPLF) imesema wapiganaji wa harakati hiyo ya kaskazini mwa Ethiopia hivi sasa wapo katika hali na nafasi nzuri ya kusonga mbele na kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Addis Ababa.
-
Jeshi la Ethiopia lasema liko tayari kulinda Bwawa la Renaissance
Jul 23, 2021 23:25Meja Jenerali Yalma Merdasa, Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Ethiopia, amesema kwamba kikosi hicho hakijatoa jicho lake kwenye Bwawa la Renaissance hata kwa dakika moja, na kwamba kiko tayari kulinda usalama wa anga wa nchi hiyo.
-
Watu 20 wauawa katika mapigano karibu na Tigray, Ethiopia
Jul 22, 2021 23:47Watu 20 wameuawa katika mapigano ya silaha yaliyojiri karibu na eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia.
-
Sudan yaionya Ethiopia kuhusu Bwawa la al Nahdha
Jul 22, 2021 06:21Waziri Mkuu wa Sudan ametoa onyo kwa serikali ya Ethioia isichukue uamuzi wowote wa upande mmoja kuhusu mgogoro wa Bwawa la al Nahdha.
-
Ethiopia yauonya Umoja wa Ulaya; yautaka usipendelee upande wowote katika mzozo wa Bwawa la al-Nahdha
Jul 21, 2021 07:40Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ethiopia amesema kuwa, nchi yake inapinga upatanishi wa aina yoyote wa Bwawa la al-Nahdha ambao upo nje ya fremu ya Umoja wa Afrika na kuuonya Umoja wa Ulaya kwamba, usipendelee upande wowote katika mzozo huo.
-
Zoezi la kumimina maji kwa awamu ya pili katika Bwawa la al Nahdha lamalizika
Jul 19, 2021 21:51Licha ya kuweko maonyo na vitisho vikali vya Sudan na Misri, lakini duru moja ya masuala ya umwagiliaji maji nchini Ethiopia imesema kuwa, zoezi la kumimina maji kwa awamu ya pili katika Bwawa la al Nahdha limekamilika.
-
Waziri Mkuu wa Ethiopia aapa kuiangamiza moja kwa moja harakati ya ukombozi wa Tigray
Jul 19, 2021 03:26Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameapa kuitokomeza moja kwa moja Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray TPLF, kundi ambalo liliwahi kuwa chama tawala nchini humo na ambalo sasa serikali ya Addis Ababa inalitambua kama harakati ya kigaidi.