-
Hamas: Mwisho wa Abu Shabab ndio hatima isiyoepukika ya kila msaliti
Dec 05, 2025 10:50Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeonya kwamba mauaji ya mshirika wa Israel na kiongozi wa genge lenye uhusiano na Daesh, Yasser Abu Shabab, ni hatima isiyoepukika ya kila mtu anayechagua kulisaliti taifa na nchi yake na kushirikiana na utawala ghasibu wa Israel.
-
Spika wa Bunge: Iran iko wazi kwa diplomasia lakini usalama wa taifa na nguvu ya ulinzi haviwezi kujadiliwa
Dec 05, 2025 02:58Spika wa Bunge la Iran, Mohammad-Baqer Qalibaf amesema ingawa Iran iko wazi kwa diplomasia, lakini haitalegeza kamba katika suala la usalama wa taifa na nguvu zake za ulinzi.
-
Foleni za watu wenye njaa huko Ghaza zimezidi kuwa ndefu + Picha
Nov 30, 2025 02:36Licha ya kusitishwa mapigano huko Ghaza, lakini bado mateso ya njaa na ukosefu wa usalama na utulivu wa nafsi yanaendelea kuzisumbua familia za Wapalestina. Foleni ndefu za watu wenye njaa wanaosubiri kupata angalau mlo mmoja kwa siku zinaendelea kuonekana katika pembe mbalimbali za ukanda huo huku jeshi katili la Israeli likiendeleza mashambulizi ya mara kwa mara na kuzuia kuwafikia misaada wananchi hao wasio na ulinzi.
-
Israel yatumia mfumo wa akili mnemba (AI) kufuatilia mitandao ya kijamii ya wanajeshi, ili kuzuia ushahidi wa uhalifu wa kivita
Nov 28, 2025 02:59Jeshi la Israel limezindua mradi mkubwa wa akili mnemba (AI), unaojulikana kama Morpheus, ili kuzuia askari wake kuchapisha ushahidi wa uhalifu wa kivita uliofanyika huko Gaza kwenye mitandao ya kijamii.
-
UNRWA: Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kuzuia misaada kwa Gaza
Nov 16, 2025 04:13Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limekosoa kuendelea kuwekewa vikwazo vya misaada katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, utawala ghasibu wa Israel kama utawala unaoukalia kwa mabavu hautekelezi wajibu wake kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu.
-
Kwa nini China na Russia zimepinga azimio lililopendekezwa na Marekani kuhusu Gaza?
Nov 16, 2025 02:26Russia na China ambazo ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimetaka kufutwa kikamilifu "Tume ya Amani" kwenye matini ya rasimu iliyowasilishwa na Marekani kwenye baraza kuhusu Gaza.
-
Maiti zingine 51 za Wapalestina waliouliwa shahidi na jeshi la kizayuni zagunduliwa Ghaza
Nov 14, 2025 07:43Timu za uokoaji za Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimegundua na kufukua maiti zingine 51 za Wapalestina waliouliwa shahidi na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel.
-
Israel yaendelea kuwatesa kwa njaa Wapalestina kwa kuruhusu 24% tu ya misaada kuingizwa Ghaza
Nov 02, 2025 06:50Mamlaka za Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimetangaza kuwa utawala wa kizayuni wa Israel umeruhusu kuingizwa katika eneo hilo sehemu ndogo tu ya misaada ya kibinadamu kinyume na ilivyoafikiwa katika makubaliano ya usitishaji mapigano yanayosimamiwa na serikali ya Marekani, ambayo yalianza kutekelezwa mwezi uliopita.
-
Jinsi himaya isiyo na masharti ya Ujerumani kwa Israel inavyoakisi unafiki wa vigezo vya Magharibi vya haki za binadamu
Nov 01, 2025 12:29Msemaji wa harakati ya Hamas amekosoa kauli za Kansela wa Ujerumani Friedrich Mertz za kujaribu kutetea uhalifu na jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina.
-
Unafiki wa Ulaya mkabala wa Gaza: Biashara na Israel au kuheshimu haki za binadamu?
Oct 23, 2025 02:29Umoja wa Ulaya utarejesha uhusiano wake wa kibiashara wa upendeleo na Israel hatua kwa hatua kwa kisingizio cha kutekelezwa usitishaji unaolegalega wa mapigano huko Gaza.