-
Mapigano makali yaripotiwa Mji wa Ghaza, askari 12 wa Israel waripotiwa kuuawa na kujeruhiwa, wanne watoweka
Aug 30, 2025 02:24Chaneli ya i24 ya utawala wa kizayuni wa Israel imeripoti kujiri mapigano makali kwenye viunga vya Mji wa Ghaza kati ya wanamuqawama wa Palestina na askari wa utawala huo ghasibu wakati askari hao wanajaribu kuuteka mji huo kupitia mashambulizi ya anga na mizinga mikubwa.
-
Sasa Uturuki yakata mahusiano yote ya kibiashara na Israel, yafunga anga, bandari kwa sababu ya Ghaza
Aug 30, 2025 02:22Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan ametangaza kuwa nchi hiyo inafunga anga na bandari zake kwa ndege na meli za utawala wa kizayuni wa Israel, na kukata kikamilifu mahusiano yote ya kiuchumi na kibiashara na utawala huo kutokana na vita vyake vya mauaji ya kimbari unavyoendeleza huko Ghaza, Palestina.
-
Zakzaky: Mipango ya kuwafukuza Wapalestina Gaza, kuipokonya silaha Hizbullah itafeli
Aug 19, 2025 07:14Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Yaqoub Zakzaky amebainisha kuwa, mipango ya utawala wa Kizayuni ya kuwaondoa kwa nguvu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza katika ardhi yao na kuipokonya silaha Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon kwa kutumia serikali ya Beirut itagonga mwamba.
-
Maandamano ya kutaka kulindwa wanahabari wa Gaza yafanyika Afrika Kusini
Aug 18, 2025 03:18Waandishi wa habari wa Afrika Kusini na wafanyakazi wa vyombo vya habari wameongoza maandamano huko Sea Point jijini Cape Town, wakishinikiza kupewa ulinzi zaidi waandishi wa habari wa Palestina huko Gaza, sanjari na kutangaza mshikamano na wenzao waliouawa katika ukanda huo wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
-
Maelfu waandamana mjini New York kupinga sera ya njaa huko Gaza
Aug 17, 2025 07:54Maelfu ya wananchi wa Marekani wameshiriki maandamano huko mjini New York kutaka kukomeshwa utumiaji wa njaa kwa makusudi dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, sambamba na kuchukuliwa hatua za haraka za kimataifa za kukomesha mauaji ya halaiki katika eneo hilo.
-
Je, nchi za Amerika ya Kusini zimepokea vipi mpango wa Israel wa kukalia kwa mabavu Gaza?
Aug 15, 2025 22:47Nchi nyingi za Amerika ya Kusini zimekuwa na misimamo ya kukosoa waziwazi mpango wa utawala wa Kizayuni wa kuikalia kijeshi Gaza. Bila shaka, baadhi ya nchi, kama vile Argentina, zimechukua msimamo tofauti wa kuiunga mkono Tel Aviv.
-
Mamilioni ya Waislamu waadhimisha Arubaini ya Imam Hussein AS katika mji mtakatifu wa Karbala
Aug 14, 2025 10:52Mamilioni ya Waislamu kutoka pembe mbalimbali za dunia wamekusanyika katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq kuadhimisha Arubaini ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), Imam wa tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW).
-
Wanajeshi wa Somalia waliokula njama na Al Shabab ya kumuua kamanda wa kikosi chao wanyongwa
Aug 12, 2025 03:27Wanajeshi wawili wa Somalia waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kula njama na kundi la kigaidi la Al Shabab ya kumuua kamanda wa kikosi chao walitekelezewa hukumu yao jana Jumatatu. Hayo ni kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka wa mahakama ya kijeshi ya nchi hiyo.
-
Jamii ya Wangazija yapiganiwa itambuliwe rasmi nchini Kenya
Aug 08, 2025 08:09Seneta wa Kaunti ya Mombasa iliyoko eneo la pwani ya Kenya ametoa wito wa kutaka suala la jamii ya Wangazija kutatuliwa na kupewa haki kama watu wengine nchini humo.
-
HAMAS yamsuta Witkoff, yasema haitaweka chini silaha mpaka iundwe nchi huru ya Palestina
Aug 03, 2025 02:12Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imekanusha madai yaliyotolewa na mjumbe wa Marekani Mashariki ya Kati Steve Witkoff kwamba ilionyesha nia ya kuwa tayari kukabidhi silaha zake wakati wa mazungumzo ya kusitisha mapigano Ghaza kati yake na Israel, ikisisitiza kwamba ina haki ya "kitaifa na kisheria" kukabiliana na uvamizi wa utawala huo wa kizayuni katika ardhi ya Palestina.