May 16, 2023 14:19
Majenerali wa jeshi la utawala wa Kizayuni wamekiri kupata pigo katika vita vya siku tano vilivyoisha Ijumaa iliyopita na kutangaza wazi kwamba, katika uvamizi wake wa hivi karibuni huko Ghaza, utawala wa Israel si tu haukupata mafanikio yoyote, lakini ngome ya ulinzi wa anga ya Israel imeshindwa kukabiliana na makombora ya muqawama wa Palestina.