-
Hamas: Asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni wameuawa katika mashambulizi ya Israel
May 18, 2024 00:30Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa mashambulizi ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ambao unakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo, yameuwa asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao walikuwa wakishikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa mwezi Oktoba mwaka jana.
-
HAMAS: Mashambulio ya Israel yameua 70% ya mateka wa Kizayuni
May 17, 2024 04:43Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, unaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo ghasibu, yameua asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao wanashikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu ilipotekelezwa operesheni ya mwezi Oktoba ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
-
Afisa wa Hamas: Muqawama wa Gaza umeweza kukabiliana kwa mafanikio na vita vya dunia
May 11, 2024 23:06Sami Abu Zuhri, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS), amesema kwamba Muqawama na mapambano ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza yamefanikiwa kukabiliana na "vita vya kimataifa," na nchi zilizoifadhili Israel sasa zinaanza kusitisha uungaji mkono wao kwa utawala huo.
-
Askari wa Israel waendelea kuangamizwa na wanamuqawama Gaza
May 11, 2024 04:29Wanajeshi wengine watano wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa katika shambulizi la ulipizaji kisasi lililofanywa na Mujahidina wa Brigedi za Izzuddin al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS katika Ukanda wa Gaza.
-
Askari 3 wa Israel waangamizwa katika shambulio la HAMAS
May 06, 2024 03:42Wanajeshi watatu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa katika shambulizi la ulipizaji kisasi lililofanywa na Mujahidina wa Brigedi za Izzuddin al-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS.
-
Jitihada za China za kuleta maridhiano ya kitaifa Palestina
May 01, 2024 23:05Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ametangaza kuwa kufuatia mkutano wa wawakilishi wa harakati za Palestina za Hamas na Fat'h mjini Beijing, pande mbili zimefikia makubaliano ya kujadili maridhiano ya kitaifa huko Palestina.
-
Blinken aitolea wito Hamas ikubali 'pendekezo barabara sana' la kusitisha vita Ghaza
May 01, 2024 07:46Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameitolea wito Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ikubali pendekezo la makubaliano ya kusitisha mapigano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Hamas: Miili ya makaburi ya umati Gaza ifanyiwe uchunguzi
Apr 26, 2024 23:17Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa wito wa kutumwa timu za uchunguzi ili kutambua miili iliyogunduliwa kwenye makaburi ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.
-
HAMAS: Shambulio la Iran ni haki ya kimaumbile na jibu linalostahiki dhidi ya Israel
Apr 14, 2024 07:41Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, shambulio lililofanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) dhidi ya utawala wa Kizayuni ni jibu la kimaumbile na linalostahiki.
-
HAMAS: Kusitishwa vita kikamilifu ndio msingi wa kufikia mapatano na utawala wa Kizayuni
Apr 12, 2024 07:47Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, usitishaji vita wa kudumu ndio msingi mkuu wa kufikia mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel juu ya kuwarejesha makwao bila ya masharti yoyote Wapalestina waliolazimika kuyahama makazi yao na kuondoka kikamilifu vikosi vya utawala huo katika Ukanda wa Ghaza.