Abbas akosolewa kwa kujidhalilisha mbele ya Waziri wa Vita wa Israel
(last modified Wed, 29 Dec 2021 07:42:14 GMT )
Dec 29, 2021 07:42 UTC
  • Abbas akosolewa kwa kujidhalilisha mbele ya Waziri wa Vita wa Israel

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amekosolewa vikali kwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hazem Qassem, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kitendo cha Abbas kwenda kujikomba mbele ya Waziri wa Vita wa Israel ni sawa na kuipiga jambia kwa nyuma kambi ya Inifadha.

Amesema mkutano huo wa Abbas na Benny Gantz, Waziri wa Vita wa Israel hautakuwa na matokeo mengine ghairi ya kushadidisha migawanyiko ya kisiasa miongoni mwa Wapalestina.

Abbas na Gantz walikutana na kufanya mazungumzo katika kikao cha faragha jioni ya jana Jumanne. Ikumbukwe kuwa, Agosti mwaka huu, Abbas alikutana tena na kufanya mazungumzo na Benny Gantz katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Hazem Qassem, Msemaji wa HAMAS

Oktoba mwaka huu, Rais huyo wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alikutana kwa siri na kufanya mazungumzo na Nitzan Horowitz, Waziri wa Afya wa utawala wa Kizayuni na mwenzake wa Ushirikiano wa Kieneo, Esawi Freij, mjini Ramallah, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Abbas anaendelea kujikomba kwa Wazayuni katika hali ambayo, Naftali Bennett, Waziri Mkuu mpya wa utawala khabithi wa Israel mwenye misimamo ya kufurutu ada amesisitiza mara kadhaa kuwa, kamwe hatoruhusu kuundwa dola la Palestina katika utawala wake.

Tags