Sep 04, 2020 07:07
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniya kwa mara nyingine tena amesisitiza udharura wa kuungana na kushirikiana makundi yote ya kisiasa na kijamii ya Palestina kwa lengo kuzima njama za maadui zao, yaani utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na baadhi ya tawala za kizandiki za Kiarabu.