-
HAMAS: Mpango wa Israel wa kupora ardhi za Ukingo wa Magharibi utagonga mwamba
Sep 24, 2020 08:29Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, njama za Marekani na utawala haramu wa Israel za kutaka kutwaa ardhi zaidi katika Ukingo wa Magharibi na kuziunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina zitashindwa na kugonga ukuta.
-
HAMAS yaipa Israel miezi 2 ihitimishe mzingiro wa Gaza
Sep 22, 2020 22:05Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeupa utawala wa Kizayuni wa Israel muhula wa miezi miwili wa kuhitimishwa mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza.
-
Mwakilishi wa Hamas Tehran: Mapambano ndiyo njia pekee ya kushinda ubeberu
Sep 15, 2020 05:55Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) mjini Tehran amesema kuwa, mapambano na mshikamano wa Umma wa Kiislamu ndiyo njia pekee ya mataifa ya kuweza kuishinda Marekani na ubeberu wa kimataifa.
-
Haniya: Marekani inajaribu kuanzisha njia za mazungumzo na Hamas
Sep 14, 2020 03:14Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema Marekani imefungua njia za kuanzisha mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu wa harakati hiyo, ili kulishawishi kundi hilo liafiki kutekeleza mpango wa 'Muamala wa Karne.'
-
Hamas: Jamii ya kimataifa ichukue hatua za kuokoa mateka wa Kipalestina katika jela za Israel
Sep 07, 2020 02:06Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeitaka jamii ya kimataifa na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu dunia kuchukua hatua za maana za kuokoa maisha ya mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel ambao wanakabiliwa na hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.
-
Hamas yakanusha madai ya kukamatwa wanachama wake 2 na Marekani
Sep 06, 2020 03:07Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imekadhibisha vikali madai kwamba Marekani imewatia mbaroni watu wawili wenye mfungamano na harakati hiyo.
-
Hamas yalaani njama za Bahrain za kuwa na uhusiano wa kawaida na Wazayuni
Sep 04, 2020 07:27Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, kitendo cha baadhi ya nchi cha kuusaidia Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel kinazidi kuutia kiburi utawala huo pandikizi cha kuendeleza jinai zake dhidi ya Wapalestina na nchi za eneo hili.
-
HAMAS yasisitizia umoja wa Wapalestina mkabala wa njama za Israel-Marekani
Sep 04, 2020 02:37Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniya kwa mara nyingine tena amesisitiza udharura wa kuungana na kushirikiana makundi yote ya kisiasa na kijamii ya Palestina kwa lengo kuzima njama za maadui zao, yaani utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na baadhi ya tawala za kizandiki za Kiarabu.
-
HAMAS yasisitiza kuendeleza uhusiano wa kistratejia na Hizbullah ya Lebanon
Sep 03, 2020 03:37Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, uhusiano wa kistratejia baina ya makundi ya ukombozi na muqawama na Hizbullah ya Lebanon utapelekea kukombolewa Palestina kutoka kwenye makucha ya maghasibu wa Israel.
-
Ismail Haniya: Azma ya muqawama Palestina ni kuhitimisha mzingiro dhidi ya Gaza
Aug 30, 2020 22:05Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, azama na irada ya taifa na muqawama wa Palestina ni kufanya hima kwa ajili ya kuhitimisha mzingiro wa kidhulma unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.