-
Shirikisho la Soka la Iran likaribisha pendekezo la Wapalestina la kuwekewa vikwazo Shirikisho la soka la Israel
Mar 25, 2024 08:14Mkuu wa Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia barua Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), akikaribisha mpango uliopendekezwa wa Shirikisho la Soka la Palestina kuhusu kuwekewa vikwazo Shirikisho la Soka la utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran na Oman zasisitizia udharura wa kukomeshwa mara moja jinai za Israel Ghaza
Mar 25, 2024 02:43Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman wamefanya mazungumzo ya simu na kutilia mkazo wajibu wa kuchukuliwa hatua za haraka na jamii ya kimataifa za kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhlumu na wasio na ulinzi wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza.
-
Wairani waandamana kulaani jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza
Mar 24, 2024 23:21Wananchi wa Iran wamefanya maandamano makubwa katika sehemu mbalimbali za nchi ukiwemo mji mkuu Tehran, kutangaza mshikamano na wananchi madhulumu wa Palestina wanaoendelea kuuawa, sambamba na kulaani jinai za kutisha zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
"Mauaji ya kimbara Gaza yamefichua dhati na unafiki wa Wamagharibi"
Mar 23, 2024 04:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mauaji ya kimbari yanayoshuhudiwa katika Ukanda wa Gaza yameweka bayana kuwa nchi za Magharibi zinatumia suala la 'haki za binadamu' kama wenzo wa kisiasa tu.
-
Msemaji wa AEOI: Iran inahitaji vituo 20 vya nyuklia
Mar 23, 2024 04:15Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema Jamhuri ya Kiislamu inapasa kuwa na vituo kati ya 15 na 20 vya nyuklia ili kujidhaminia mahitaji yake ya nishati.
-
Iran yalaani shambulizi la kigaidi lililoua makumi ya watu nchini Russia
Mar 22, 2024 23:21Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali shambulio la kigaidi lililoua na kujeruhi makumi ya watu katika mji mkuu wa Russia, Moscow.
-
Iran yalaani kimya cha dunia mkabala wa jinai za Israel huko Gaza
Mar 21, 2024 07:35Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito wa kusitishwa uungaji mkono kwa jinai na mauaji yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Njia ya kukomesha dhulma kubwa ya kuwepo utawala wa Kizayuni itaendelea
Mar 20, 2024 23:30Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema: Njia ya kukomesha dhulma kubwa ya kuwepo utawala wa Kizayuni wa Israel itaendelea.
-
Iran yaonya kuhusu hatua za Wazayuni dhidi ya Wapalestina wanaokwenda kusali Msikiti wa Al-Aqsa
Mar 20, 2024 08:41Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametahadharisha kuhusu vitendo vyovyote vya kichokozi vinavyoweza kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Quds Tukufu na Msikiti wa Al-Aqsa dhidi ya Waislamu Wapalestina wanaokwenda kusali katika msikiti huo wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Iran: Shutuma za USA na UK kuhusu Bahari Nyekundu na Yemen hazina msingi wowote
Mar 19, 2024 04:27Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha tuhuma zisizo na msingi za Marekani na Uingereza dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu hali ya Bahari Nyekundu na Yemen.